Featured Post

VIJANA WANUFAIKA NA UJASIRIAMALI

Kutoka Kushoto Muweka hazina wa Kikundi cha Jikomboe Salum Nampaya akitoa Maelezo Kuhusiana na Uvunaji wa asali kwa Viongozi wa Africare Walipotembelewa Mtaa wa Lwelu Manispaa ya Mtwara Mikindani ambapo tangu walipoanza kikundi kilikuwa na Mizinga Mitano kwa ajili ya ufugaji nyuki lakini kwa sasa wameweza kuwa na Mizinga Sitini {60} ambapo wanaweza kuvuna Asali Lita Miambili na Ishirini 220}.
JOSEPH MPANGALA , MTWARA

Zaidi ya Vijana 200 wa Mkoa wa Mtwara wameunufaika na Ujasiliamali Kupitia Mradi wa KIJANA JIKWAMUE unaotekelezwa na Shirika la Africare na kufadhiliwa na Kampuni ya Uchimbaji na Uzalishaji Nishati ya Gas na Mafuta ya Shell.

Vijana hao waliopo katika Makundi 12 ambapo wanajishulisha na Ufugaji wa nyuki,Ufugaji wa Kukubora,Kilimo,Biashara Ndogondogo pamoja na kuongeza thamani Bidhaa mbalimbali na kuzitafutia masoko kwe lengo la kujipatia Kipato cha kila siku.

Frank Lyimo meneja Mradi anasema Mradi umeanza kuonesha mafanikio kutokana na baadhi ya Vikundi wameanza kuzalisha Bidhaa Bora ambazo zimeonekana kuwa na Ushindani katika Masoko tofauti kutokana na Kupata Vifungashio Bora na vyenye Nembo inayovutia.

“Mradi wa Kijana Jikwamue Unashughulika na kuwajengea uwezo wajasiliamali ambo kwa sasa umeonesha mafanikio kutokana na baadhi ya vikundi wanaweza kuzalisha Bidhaa Bora kwa mfano kuna kikundi kinafuga Kukumiatano mpaka Elfmoja ambao wanapelekwa sokoni wafikapo kuanzia kilo 1.3 na Tumewawezesha mabanda ya kutosha lakini wengine wanaongeza thamani Kilimo cha Mboga mboga pamoja na Asali” amesema Frank.

Naye Mshauri Muandamizi Maswala ya Jamii wa kampuni ya Shell Msomisi Mbenna anasema Kunaonekana kuwa na mafanikio kutoka Mradi wa awam ya kwanza na sasa awam ya Pili ambapo lengo kubwa ni kuwawezesha kupanua Biashara ili kuweza kupata masoko sio tu kwa mkoa wa Mtwa balinchi Nzima.

“Nimefurahi sana kutembelea miradi hii na kuona manufaa ambayo Wananchii wameyapata kutoka kwenye awam ya kwanza na sasa hivi awam ya Pili na Tunaimani kuwa kwenye hii awam ya Pili watu watapata mafunzobora zaidi na waweze kupata masoko kwa sababu lengo la Awam ya Pili ni kuwawezesha waweze kupanua Biasha na kupata masoko Nje ya Mkoa wa Mtwara”

Abdulah Mkumbila ni mmoja wa wajumbe kutoka kikundi cha Jikomboe Kilichopo Mtaa Lwelu Manispaa ya Mtwara Mikindani anasema walianza na Mizinga mitano{5} kwa ajili ya kufuga Nyuki lakini kwa sasa wanamizinga Sitini{60}ambayo inaweza kuzalisha Asali Lita Miambili na Ishiriri{220}

“ Kutokana na Kupata Mizinga hii tayari baadhi ya wajumbe wameweza kujenga Nyumba Bora kwa utaratibu wa kukopa pesa na kurejesha na wengine wamenunua Pikipiki lakini Bado Kikundi kipo kwenye Mchakato wakuongeza Miradi Mingine kama Vile Ulimaji wa Bustani za Mboga Mboga ili kuongeza kipato”
Mshauri Muandamizi Maswala ya Jamii wa kampuni ya Shell Msomisi Mbenna akitoa Ufafanuzi Kuhusiana na Ushiriki wa kampuni yake katika Mkutano kamati ya utendaji ya mradi wa Kijana Jikwamue Unaoendeshwa na Shirika la Africare na Kufadhiliwa na Kampuni ya Shell Mkutano Ulifanyika Mkoani Mtwara 
Wajumbe wa kamati ya Utendaji wa Mradi wa Kijana Jikwamue Wakiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya Kumaliza Kikao cha kupokea Taarifa za Mradi wa Awam ya Kwanza pamoja na Mapendekezo na Mpango kazi wa Mradi kwa awamu ya Pili kwa ajili ya kuwawezesha Vijana wa Mkoa wa Mtwara 
Mshauri Muandamizi Maswala ya Jamii wa kampuni ya Shell Msomisi Mbenna akipokea Taarifa ya Utendaji Kutoka kwa Abdulah Mkumbila ambaye ni Mjumbe wa Kikundi cha Jikomboe Kilichopo Mtaa wa Lwilo ambacho kinajishughulisha na Uzalishaji wa Asali Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Shirika la Africare Alfred Kalaghe. 

Comments