Featured Post

JAMII FORUMS WAIBUKIA NCHINI KENYA BAADA YA KUFUNGWA TANZANIA

Sheria hiyo inadaiwa kulenga kuwanyamazisha wanahari nchini humo

Image captionSheria hiyo inadaiwa kulenga kuwanyamazisha wanahabari nchini Tanzania
Mtandao maarufu nchini Tanzania wa Jamii Forums ambao ulisitisha huduma zake kutokana na sheria za serikali za kudhibiti mitandao sasa unaweza kupatikana tena.

Mtandao huo ni maarufu kwa kifichua mambo tofauti na kama jukwaa la watu kutoa maoni haswa wale walio nchini Tanzania na nchi za kigeni, sasa unapatikana kupitia mtandao wa Kenya (kenyatalk.com).
Waliokuwa wakiutumia mtandao wa Jamii Forums kabla ufunge, wanaweza kuendelea kuutumia kwa kujisajili kupitia ule wa KenyaTalk ambao ulijitolea kutoa huduma hizo kwa niaba yake.
Hata hivyo idadi ya watu amboa wanatembela mtandao huo bado ni ya chini kutokana na sababu kuwa wengi hawajafahamu ikiwa bado unapatikana au njia ya kuufikia.
Akiongea na gazeti na Citizen la Tanzania mwanzilishi wa Jamii Forums Maxence Melo, anasema anafahamu kuhusubh hilo lakini akakana kuipa KenyaTalk ruhusa ya kutoa huduma zake.
Jamii Forums unaibuka tena siku tatu baada kufungwa nchini Tanzania kufuatia sheria zilizotangazwa na halmashauri ya mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) ambazo waanzilishi wa Jamii Forums walizioana kama zilizowalenga.
Mambo muhimu kuhusu kanuni za mitandao Tanzania
Image captionMambo muhimu kuhusu kanuni za mitandao Tanzania
Sheria hizo mpya za TCRA ziliwahitaji wachapishaji wa mitandao na wanablogi kufichua wachangiaji na wamiliki kitu ambacho Bw Melo anasema kuwa ni kizingiti kwa kazi yao.
Kupitia mtandao wa Kenya wa KenyaTalk, watumiaji wa Jamii Forums waliojiandikisha wanaweza kuchangia maoni yao vile walivyokuwa wanachangia awali.
Siku ya mwisho iliyotangazwa na TCRA ya kuwataka wamiliki wa mitandao kujiandikisha na kupata leseni ni Ijumaa tarehe 15 mwezi huu lakini halmashauri hiyo imesema kuwa haitafunga mitando ambayo itakosa kutimizia sheria hiyo hapo kesho.
Lakini mitandao hiyo itapigwa mafuruku kuchapisha taarifa zozote mpya hadi ikamilishe shughuli ya kujiandikisha.

Comments