Featured Post

WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR WAISHAURI WIZARA YA ELIMU KUBORESHA MIUNDO MBINU KATIKA SKULI ZOTE

WAT4
MWASHUNGI TAHIR NA FATMA MAKAME         MAELEZO ZANZIBAR
 Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameshauri Wizara ya Elimu kuboresha miundo mbinu katika maskuli kwa ajili kuboresha miundo mbinu kwa watu wenye ulemavu li kuwapatia wepesi watu hao.
Wakichangia bajeti ya makadirio ya mapato ya Serikali 2018- 2019   ya Wizara ya Elimu wameitaka Wizara hiyo kuweka miundo mbinu kwa ajili ya watu wenye  ulemavu ili kuondoshea usumbufu  watu hao.

Aidha walisema kuweko kwa miundo mbinu hiyo kutaweza kuwapa urahisi watu wenye ulemavu katika maskuli na kuweza kujipatia elimu kwa urahisi ambao na wao wanahitaji mambo yao ya msingi ikiwemo elimu..
Vile vile waliishauri Wizara kuweka mafundi wenye vigezo  katika kujenga maskuli ili skuli ziwe na kiwango  na sio kutafutwa mafundi wasio na vigezo na baada ya muda mfupi majengo yakawa hayafai  .
Pia wameiomba wizara kuweka kamati maalum ya kuchunguza majengo mbali mbali ya Skuli za Serikali kutokana na hitilafu zinazoweza kujitokeza kwenye majengo hayo licha ya kuwa mapya.
Wajumbe hao wameiomba Wizara ya elimu kuwabadilishia mishahara walimu waliojiojiongezea elimu ikiwemo kiwango cha digrii na masta , kwani wanakaa muda mrefu hawajabadilishiwa mishahara baada ya kumaliza kusoma.
Hivyo wameiomba Wizara ifanye haraka kuwabadilishia mishahara walimu hao   ili wapate kuwapa moyo na wale wanaojipanga kwenda kusoma wawe na motisha wa kwenda kujiongezea elimu na kuweza kupata walimu wenye elimu ya juu ili na wao wafanye kazi zao kwa ufanisi.

Comments