Featured Post

TNBC YASAINI MKATABA WA UBORESHAJI MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI (LIC )

8H3H0599
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Raymond Mbilinyi na Kiongozi wa Mradi wa LIC Flemming Winther Olsen wakiweka saini ya Mkataba wa kazi wa Uboreshaji mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini. Mikataba hiyo imesainiwa  tarehe  22 Mei 2018 katika ofisi TNBC Tan House  Jijini Dar es Salaam.

8H3H0607
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Raymond Mbilinyi na Kiongozi wa Mradi wa LIC Flemming Winther Olsen wakibadilishana mikataba baada ya kusaini makubaliano ya kazi baina yao  katika Ofisi za TNBC Tan House Jijini Dar es Salaam Mei 22,2018.
8H3H0653
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara TNBC Raymond Mbilinyi akizungumza na waaandishi wa habari baada ya kusaini Mkataba wa kazi na Mradi wa uboreshaji mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini  (LIC) unaofadhiliwa na Nchi ya Denmark . Kulia ni Kiongozi wa Mradi wa LIC Flemming Winther Oslen. 
8H3H0689
Kiongozi wa Mradi wa LIC Flemming Winther Oslen akiwaelezea waandishi wa habari dhumuni la ufadhili wa mradi huu kwa TNBC ni kutaka kuiinua sekta binafsi zaidi na kuipa nguvu kuweza kushirikiana na serikali katika kuinua uchumi wa nchi. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa TNBC Raymond Mbilinyi.
……………..
Baraza la Taifa la Biashara TNBC imesaini mkataba na Mradi wa Uboreshaji Mazingira ya Biashara na Uwekezaji ( LIC)  kwa awamu ya nne kuanzia Mei 2018 hadi Februari 2020 katika mikoa ya Kigoma na Dodoma kama mradi wa mfano.
Akizungumza na waandishi wa Habari ofisi kwakwe Jijini Dar es salaam Katibu  Mtendaji Raymond Mbilinyi alisema Mradi wa LIC umeweza kusaidia masuala ya biashara katika mabaraza ya Wilaya  ikiwa ni pamoja na  kuunganisha Taasisi za Sekta ya Binafsi ili kuweza kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa masuala ya uwekezaji nchini.
Lengo la mradi huu, ni kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa njia ya majadiliano, kuongeza ajira na fursa za kipato kwa wakulima na wajasiriamali wadogo wadogo na wakati pamoja na kuboresha hali ya ukuaji wa biashara na uwekezaji katika mikoa na Wilaya zote nchini, alisema Mbilinyi.
Mradi huu unatekelezwa katika Mikoa yote Tanzania bara, ikiwa Kigoma na Dodoma ndio Mikoa ya Mfano yaani “Modals” . Hivyo Mradi huu katika Wilaya zote za Dodoma na Kigoma umeweza kufanya vizuri, na utekelezaji huo umeweza kufanikiwa zaidi kwa kujengwa kwa  kituo cha pamoja cha kupatia huduma yaani One stop Center ambapo  mfanyabiashara anapata huduma zote katika kituo hicho ukihitaji huduma za bwana afya, Misitu, Afisa Ardhi  huduma hizo zote zinapatikana, alisisitiza Mbilinyi.
 Mradi umeanza kwa utekelezaji katika Mikoa miwili ya Kigoma na Dodoma wakiangaliza zaidi katika   kuboresha Miundombinu kwa mkoa wa Kigoma  tayari mradi huu umeweza kuboresha  mfumo wa umwagiliaji ikiwa ni pamoja na kuboresha mabwawa ya maji, ujenzi wa Soko la Kibirizi, sehemu za kuanikia samaki pamoja na sehemu za kutengezea barafu na kwa Mkoa wa Dodoma mradi huu unaendelea kuboresha Kilimo cha zao la zabibu, ”alisema Mbilinyi.
 Mradi wa LIC kwa kushirikiana na TNBC umeweza kuimarisha majadiliano baina Sekta ya Umma na binafsi kupitia mabaraza ya biashara ya mikoa na wilaya katika miradi ya ushirikiano yaani (PPP) pamoja na kusaidia kuibua na kushughulikia agenda za mabadiliko katika mazingira ya uwekezaji na biashara, ambapo majadiliano haya yameweza kuboresha makusanyo ya mapato ya Mamalaka za Serikali za Mitaa bila kusababisha kero kwa sekta binafsi.
Kiongozi wa Mradi wa LIC Flemming Winther Olsen alisema kuwa lengo kuu la mradi huo kusaini Mktaba tena na TNBC kuipa nguvu Sekta Binafsi kuendelea kukuza uchumi nchini na kuipa uwezo wa kufanyakazi kwa ufanisi kwa kushirikiana na serikali.
“Nia yetu ni kuitangaza Sekta binafsi iweze kufahamika kwa ufasaha na malengo yake yaweze kujulikana na kusaidia kushiriki katika ngazi za maamuzi ikiwa ni pamoja na kuwepo na ushirikiano  wa kufanya kazi pamoja na serikali”, alisisitiza Winther.
Baraza la Taifa la Biashara  (TNBC) kwa kushirikiana na, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Raisi Tamisemi, TPSF, kuhakikisha kwamba mikoa yote watakua na muongozo utakaosaidia majadiliano ya baina sekta binafsi na sekta ya umma yanafanikiwa kwa kupitia ufadhili wa Denmark.

Comments