Featured Post

SERIKALI WILAYANI KARATU YAJA NA MKAKATI MADHUBUTI WA KUOKOA ZIWA MANYARA KUKAUKA

Mhifadhi Mkuu wa hifadhi ya Ziwa Manyara,Noelia Mhonga akizungumza na wanahabari ofisini kwake juu ya mkakati walionao wa kuhakikisha ziwa Manyara linaendelea kuwa na maji nyakati zote.




Baadhi ya waandishi wa habari ambao wanafanya uchunguzi kubaini athari za kijamii katika eneo la ikolojia ya hifadhi ya Manyara na Tarangire wakimsikiliza mkuu wa hifadhi ya ziwa Manyara ofisini kwake


Mhifadhi ujirani mwema wa hifadhi ya Manyara, Ibrahim Ninga akizungumza na wanahabariwanaofuatilia kujua athari za kijamii kuzunguka eneo la ikolojia ya hifadhi ya ziwa Manyara na Tarangire


Mkuu wa wilaya ya Karatu, Telesia Mahonga akizungumza na wanahabari juu ya mkakati wa kuzuia uharibifu unaofanywa na shughuli za binadamu katika vyanzo vya maji vinavyopeleka maji ziwa Manyara


Mwenyekiti wa kijiji cha Kilimamoja, Israel David akizungumza na wanahabari hao

Mwenyekiti wa kijiji cha Huduma Leonard Panga akizungumza na wanahabari hao

Dereva na muongoza watalii JUMANNE IDDI akizungumzia uharibifu ziwa manayara unaosababishwa na mmomonyoko wa ardhi  kutokana na shughuli za kilimo na ufugaji unaopelekea kujaa kwa tope katika ziwa hilo, hali inayotishia kukauka kwa ziwa na kupoteza mvuto na viumbe hai wanaotegemea uwepo wa ziwa hilo

Bango linaloelekeza kuingia katika hifadhi ya ziwa manyara

Charles sylvester meneja wa chemchem  foundation akizungumza na wanahabari hao


Mkurugeni wa chemchem foundation Ricardo Toss akizungumza na wanahabari hao juu ya changamoto zinazotokana na shughuli za jamii katika maeneo hayo

    
 -Wahifadhi waomba ushirikiano na wizara saba kutatua tatizo
NA: ANDREA NGOBOLE, PMT

Serikali wilaya ya Karatu, imetangaza mkakati ya kuzuia kutoendelea kujaa tope hifadhi ya ziwa Manyara kwa kuhimiza wakulima wanaolima kando ya miti inayopeleka maji katika ziwa hilo kuacha kilicho ambacho kina athari kwa hifadhi hiyo,

Hatua hiyo, imetangazwa na Serikali, ili kunusuru Hifadhi ya ziwa Manyara ambayo ipo hatarini kupotea kutokana na sehemu kubwa kujaa tope na hivyo, kuathiri mazalia ya ndege na wanyama pori.

Akizungumza na waandishi wa habari ambao wanafanya uchunguzi kubaini athari za kijamii katika eneo la ikolojia ya hifadhi ya Manyara na Tarangire, Mkuu wa wilaya ya Karatu, Telesia Mahonga alisema,kama wasipochukuwa hatua sasa, hifadhi ya ziwa Manyara itatoweka.

"sehemu kubwa ya maji katika ziwa Manyara, yanatoka Karatu maeneo ya Mbulumbulu, Kilimatembo,Bugery, Rothia na maeneo ya jirani,sasa kuna wakulima bado wanalima kilimo ambacho kinaathiri ziwa kwani tope zinaingia ziwani"alisema

Alisema katika hatua za awali, tayari ofisi yake imeanza kuchukuwa hatua kwenda vijiji kutoa elimu ya kilimo cha makinga maji,kuacha kulima kwenye vyanzo vya maji na ambao watakaidi hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwepo kuwaondoa.

Akizungumzia tatizo hilo,Mhifadhi Mkuu wa hifadhi ya Ziwa Manyara,Noelia Mhonga alisema bila jitihada za haraka kuchukuliwa na wizara mtambuka kunusuru ziwa hiyo, hifadhi hiyoiliyo anzishwa mwaka 1960  itatoweka.

"ni Vizuri Wizara ya tawala za mikoa za serikali za mitaa, wizara ya Maendeleo ya mifugo na Uvuvi,wizara ya maji, wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya nchi ofisi ya makamu wa Rais Mazingira na wizara ya Maliasili na Utalii, kushirikiana kupata suluhu juu ya hifadhi hii"alisema

Alisema tayari Makatibu wakuu wa wizara hizo, walitembelea hifadhi hiyo na kujionea athari za shughuli za kijamii, ikiwepo kilimo, uvuvi, uchimbaji madini na uvamizi wa mapito ya wanyama vinavyoathiri hifadhi hiyo.

Mhifadhi ujirani mwema wa hifadhi ya Manyara, Ibrahim Ninga alisema hifadhi hiyo, inazungukwa na vijiji 46 hivyo kutokana na ongezeko la shughuli za kibinaadamu, mifugo na watu hifadhi ipo hatarini.

"tunajitahidi kutoa elimu vijiji hadi kuelekeza kilimo cha kisasa,kuacha tabia ya kuzuia maji kuingia mtoni,  kuzuia uvamizi vyanzo vya maji na kuingiza mifugo hifadhini lakini tatizo ni kubwa"alisema

Mwenyekiti wa kijiji cha Kilimamoja, Israel David na Mwenyekiti wa kijiji cha Huduma Leonard Panga, walisema tatizo  la kilimo kinachoathiri ziwa Manyara ni kubwa na kupitia sheria ndogo ndogo za vijiji wanalishughulia.

"wananchi wanagoma kuondoka kulima pembezoni mwa mito,tunatoa elimu lakini wengi wagumu na tunaomba ushirikiano mkubwa na serikali"alisema David.

Comments