Featured Post

RC TABORA AZINDUA BODI MPYA YA PAROLE

1
NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
MKUU  wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameitaka Bodi  mpya ya Parole ya Mkoani humo kutekeleza  majukumu yake kwa uadilifu kwa lengo la kupunguza wafungwa ambao idadi yao ni kubwa ukilinganisha na uwezo wa magereza.

Alisema wajumbe wanapaswa kufanya kazi kwa uadilifu huku akiitaka jamii kuwapokea watu wote wa wanaotimiza vigezo vya Parole na sio kuwanyanyapaa wanapokuwa wamerejea katika jamii zao.
Mwanri alitoa kauli hiyo jana mjini Tabora wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Parole ulifanyika katika Gereza Kuu la Uyui.
Alisema watu wanapaswa kuwapoekea na sio kuwanyanyapaa kwa vile tayari wanakuwa ni watu waliobadilika kitabia na kuwa na mwenendo mzuri.
Mwanri  alisema inapaswa Bodi hiyo kubadilika katikautendaji wake wa kazi kwa vile hata utendaji kazi wa Serikali ili waweze kwenda na kasi ya Rais Dk John Magufuli  ambaye anafanya kazi nzuri ya kupiga vita rushwa na kupambana na ufisadi.
Alisema Bodi hiyo  ikifanya kazi nzuri itasaidia kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani na kuwapeleka kufanyakazi katika jamii.
Aliipongeza Bodi iliyomaliza muda wake kwa kutoa wafungwa ishirini katika kipindi cha miaka mitatu iliyofanya kazi huku akiitaka bodi mpya kuendeleza mazuri yaliyofanywa na bodi ya zamani.
Kwa upande wa Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Tabora Hamza Rajabu alisema mpango wa Parole unatoa fursa kwa wafungwa kutumikia adhabu zao wakiwa nje ya magereza na hivyo kupunguza msongamano magerezani.
 Alisema  kuwa wanawapa mafunzo mazuri wafungwa ili wanapotoka kifungoni wawe raia wema katika jamii wanayoenda kuishi nayo.
Rajabu aliongeza kuwa  wote wanaotoka kwa mujibu wa Parole wanakuwa wamechunguzwa kikamilifu ili wawe ni watu waliojirudi kimwenendo na kuwa na tabia njema.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Timothy Sichilima alisema wakati wakitumia Bodi hiyo watazingatia uadilifu katika kutekeleza majukumu yao.
 Bodi hiyo mpya yenye wajumbe kumi na nne,itakuwa madarakani katika kipindi cha Miaka mitatu ijayo.

Comments