Featured Post

NCHI ZA AFRIKA ZATAKIWA KUFANYA MAPINDUZI YA UCHUMI KWA KUWEKEZA KWENYE VIWANDA NA MIUNDOMBINU

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Dkt. Akinwumi Adesina, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis. Shaaban wakati wa Mkutano wa 6 wa jukwaa la ushirikiano kati ya Jamhuri ya Korea Kusini na Magavana wa nchi za Afrika  Jijini Busan-Korea Kusini.

Magavana wa nchi za Afrika wametakiwa kuwa na utayari wa kuzisaidia nchi zao kutatua changamoto za kiuchumi na kuhamasisha maendeleo endelevu ili kuendana na mapinduzi makubwa yanayotokea kote Duniani kwa kuhamasisha ukuaji wa viwanda.
Rai hiyo imetolewa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina, wakati wa Mkutano wa 6 wa jukwaa la ushirikiano kati ya Jamhuri ya Korea Kusini na Nchi za Afrika uliolenga kujadili namna bora ya kuchochea ukuaji wa sekta ya viwanda katika Nchi za Afrika.
Wadau wa Mkutano huo uliofunguliwa na Makamu wa Waziri Mkuu wa Korea Kusini  Bw. Kim Dog – Yeon, wamezitaka nchi za Afrika  kuhakikisha zinafanya mapinduzi  ya kiuchumi kwa  kuwekeza kwenye viwanda na miundombinu kwa kuwa  itasaidia uchumi wa nchi kukua kwa kasi na  kuleta maendeleo yenye tija.
Vilevile nchi za Afrika zinahitaji kuwa na na ushirikiano wenye manufaa na wahisani ikiwemo nchi ya  Jamuhuri ya Korea Kusini ili kuharakisha maendeleo hayo ya kiuchumi kwa kubadilishana uzoefu na kubaini fursa za ukuaji wa uchumi utakaochochea ushirikiano huo.
Afrika inafursa nyingi za kukuza uchumi kwa kuwa inarasilimali za kutosha kwa takribani sekta zote muhimu za maendeleo ikiwemo ya madini, kilimo, mifugo na Uvuvi.
Makamu wa Waziri Mkuu wa Korea ya Kusini Mhe. Kim Dog – Yeon (wa tatu kulia ) akiwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Dkt. Akinwumi Adesina (kushoto) wakati wa majadiliano ya fursa na changamato mbalimbali zilizopo nchi za Afrika, Jijini Busan- Korea Kusini
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis. Shaaban (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Magavana kutoka nchi za Afrika kwenye Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea Kusini na nchi za Afrika, Jijini Busan- Korea Kusini. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango- Korea Kusini)
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango

Comments