Featured Post

KITENGO CHA USAID CHA KUKUZA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATIKA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI CHAZINDUA TATHMINI YA SERA ZA UWEKEZAJI TANZANIA KWA MWAKA 2018 ILI KUCHOCHEA, KULINDA NA KUENDELEZA UWEKAZAJI KUTOKA NJE

index
Dar es salaam, Tanzania 
Kitengo cha Shirika la Kimarekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) cha Kukuza Biashara na Uwekezaji katika nchi za Afrika Mashariki (East Africa Trade and Investment Hub) kimezindua Taarifa ya Tathmini ya Sera za Uwekezaji za Tanzania kwa mwaka 2018 (Tanzania Investment Policy Assessment 2018) ikiwa ni sehemu ya Jukwaa la Marekani na Tanzania lililoangazia Sera na Ubunifu lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Tathmini hii itawasaidia watengeneza sera, wakala wa mabadiliko na wawekezaji wanapofanya kazi pamoja kuhimiza, kuchochea, kulinda na kuongeza zaidi kiwango cha uwekezaji wa wawekezaji kutoka nje (FDI) nchini Tanzania.
“Kwa kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi, Tanzania inaweza kutatua changamoto zake za kimiundombinu na kukidhi mahitaji yake kama vile upatikanaji wa nishati ya gharama nafuu kwa wote na uendelezaji wa mtandao wa usafirishaji na wakati huo huo ikijenga uwezo wa watu wake, ambao ndio watakaoifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati na hata kupiga hatua kubwa zaidi ya hapo,” alisema Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dr. Inmi Patterson.
Serikali ya Marekani imedhamiria kwa dhati kushirikiana na Serikali na watu wa Tanzania ili kuimarisha na kuboresha mazingira ya kisheria na kiusimamizi wa uwekezaji kutoka nje ili kujenga Tanzania imara na yenye ustawi zaidi.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Ofisi ya Habari ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kwa simu namba: +255 22 229-4000 au kwa barua pepe: DPO@state.gov.
###
Taarifa: USAID na Kitengo cha USAID cha Kukuza Biashara na Uwekezaji katika nchi za Afrika Mashariki (The East Africa Trade and Investment Hub)
Shirika la Kimarekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) ni shirika kubwa la kimataifa la maendeleo la Serikali ya Marekani linalofanya kazi kwa ubia na Serikali ya Tanzania, serikali nyingine katika kanda, taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali na hata sekta binafsi  ili kuondoa umasikini uliokithiri, kukuza jamii zenye uwezo wa kujiletea maendeleo na za kidemokrasia na wakati huohuo kuimarisha usalama na ustawi. www.usaid.gov
Kitengi cha USAID cha Kukuza Biashara na Uwekezaji katika nchi za Afrika Mashariki (East Africa Trade and Investment Hub) hukuza biashara na uwekezaji kati ya Marekani na Afrika na baina ya nchi za Kiafrika kwa kuimarisha utangamano wa kikanda, kuongeza uwezo wa kiushindani katika mnyororo wa thamani wa mazao kadhaa ya kilimo, kukuza biashara ya pande mbili na Marekani chini ya mpango wa AGOA na kuwezesha uwekezaji na upatikanaji wa teknolojia zitakazoweza kukuza biashara ndani ya kanda na katika masoko ya kimataifa. www.eatradehub.orginfo@eatradehub.org

Comments