- Get link
- Other Apps
Featured Post
WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO WA KWENYE ZOEZI LA UANDIKISHAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA UNAOENDELEA NCHINI
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- Other Apps
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ya Nchi Mhe.Dr. Mwigulu Lameck Nchemba
akiwasili kwenye viwanja vya Shujaa Morogoro kwenye sherehe za uzinduzi wa
Zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu kwa mkoa huo. Hapa anasalimiana na
Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mstahiki Paschal Kihanga.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dr. Kebwe Steven Kebwe akisoma taarifa kuhusu
mkakati wa mkoa kuwasajili wananchi zaidi ya 960,000 wakati wa sherehe za
Uzinduzi wa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa.
Mbunge wa Morogoro Mjini Mhe. Aziz Abood
akitoa salamu kwa wananchi waliofurika kushuhudia sherehe za Uzinduzi wa zoezi
la Usajili Vitambulisho vya Taifa Morogoro.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Dr. Mwigulu Lameck Nchemba akihutubia wananchi
wakati wa Uzinduzi wa zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu wenye lengo la Kutoa
Vitambulisho vya Taifa Morogoro.
Waziri Mwigulu akiwa ameambatana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Ndugu Andrew
Massawe kukagua mashine
zitakazotumika kukusanya taarifa za wananchi wakati wa uzindizi wa zoezi la
Usajili kwa mkoa wa Morogoro.
Mhe. Waziri (Katikati) akizindua rasmi
kuanza kwa Usajili Vitambulisho vya Taifa mkoani Morogoro. Wengine ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr. Kebwe Steven
Kebwe (Wa kwanza kulia), Mbunge wa Morogoro Mjini Mhe. Aziz Abood (Wa pili
kulia), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Ndugu
Andrew Massawe (watatu kulia), Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Morogoro Mhe. Pascal Kiyanga ( wa pili kushoto) na Mkuu wa
Wilaya ya Morogoro Mhe. Regina Chonjo (wa kwanza kushoto).
Mhe Waziri wa Mambo ya Nchi pamoja na viongozi wengine wakishuhudia mmoja wa
wananchi Bi. Rehema Abdallah akisajiliwa kwa mara ya kwanza na taarifa zake
kuingizwa moja kwa moja kwenye mfumo wa NIDA wakati wa sherehe za Uzinduzi
Vitambulisho vya Taifa mkoani Morogoro.
Pamoja na kuzindua kuanza kwa zoezi la Usajili Vitambulisho mkoani Morogoro
Waziri Mwigulu pia alizindua kuanza kutolewa Vitambulisho kwa wananchi ambao
wamekamilisha taratibu za Usajili. Hapa
anamkabidhi Bi. Jackline Kayombo kitambulisho chake.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dr. Mwiguli
Lameck Nchemba awewataka watanzania kuwa wazalendo wa kweli kwenye Usajili wa
Vitambulisho vya Taifa unaoendelea kwenye mikoa 19 ya Tanzania kwa kuwafichua
wale wote wanaojipenyeza kutaka kusajiliwa kama Raia.
Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizindua shughuli za
Usajili na Utambuzi wa Watu katika Mkoa wa Morogoro Jumamosi katika viwanja vya
Shujaa mkoani humo na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ndugu Andrew Massawe
akisoma taarifa ya zoezi la Usajili na Utambuzi
wa Watu kwa mikoa 19 inayoendelea na Usajili; amesema mkoa wa Morogoro
unakusudiwa kusajiliwa zaidi ya wananchi 960,000 wenye umri wa miaka 18 na kuendelea. Zoezi ambalo limepangwa
kukamilika kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili,2018.
“ Mkoa wa Morogoro zoezi litahusisha Wilaya zote
isipokuwa Kilombero ambayo ilikuwa Wilaya ya kwanza ya mfan kufanyiwa usajili
mwaka 2012 na hivyo idadi kubwa ya wananchi wake tayari wana Vitambulisho vya
Taifa na kwasasa wanaosajiliwa ni wale wanaotimiza umri wa miaka 18 na
wanaohamia “ asisisitiza
Aidha ndugu Massawe amemweleza Mhe. Waziri mbali
na Usajili Mamlaka kwa kushirikiana na wadau wengine imeanza matumizi ya
Vitambulisho vya Taifa ikiwemo Usajili wa Makampuni unaofanywa na Brella ambao
kwa sasa unataka kila anayesajili Kampuni kuwa na Kitambulisho cha Taifa.
Huduma nyingine ambazo kwa sasa huwezi kuzipata bila kuwa na Kitambulisho cha
Taifa ni upatikanaji wa Hati za kusafiria(Passport), Usajili wa namba za simu
na huduma nyingine za kifedha n.k
Katika hotuba yake Mhe. Waziri amekemea vikali
tabia ya baadhi ya watendaji na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji kudai posho au kuhusisha
michango na tozo mbalimbali wakati wa kuwasajili wananchi wakati zoezi hilo ni
bure. Amesisitiza Mamlaka zote za
Serikali kuhakikisha zinasisimia na kutoa ushirikiano kwa NIDA kuhakikisha
wananchi wote wenye sifa wanasajiliwa kwa wakati wakiwemo Wageni na Wakimbizi
kwani shughuli ya usajili kwa sasa inahusisha makundi yote. Pindi wakati utakapofika kwa wale wote ambao
watakuwa hawakusajiliwa watakuwa na cha kujieleza kwanini hawakusajiliwa
Vitambulisho vya Taifa wakati Serikali imewekeza fedha nyingi kukamilisha zoezi
hili.
Amesisitiza Usajili Vitambulisho vya Taifa si
hiyari ni wajibu wa kila Raia, Mgeni na Mkumbizi kusajiliwa kwa kufuata
taratibu, sharia na kanuni za Usajili zinazosimamiwa wakati wa utekelezaji wa
Usajili.
“ Kama mnavyofahamu Serikali ya Awamu ya Tano
chini Mhe. Dr. John Pombe Magufuli ina vipaumbele vingi na mahitaji kwa
wananchi ni mengi. Sasa Rais ameacha mambo mengine akaamua kuwekeza kwenye
Vitambulisho vya Taifa mradi unaoigharimu Serikali fedha nyingi sana; sasa ole
wao ambao hawatasajiliwa kwa visingizio visivyokuwa na msingi” alisisitiza
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dr.
Kebwe Steven Kebwe amewataka wananchi wa Morogoro kujitokeza kwa wingi kwenye
Usajili wa Vitambulisho vya Taifa unaoendelea maeneo mbalimbali ya mkoa huo na
kusisitiza hatowafumbia macho wale wote watakao husisha zoezi hilo na itikadi
za vyama au dini, au kudai rushwa kuwahudumia wananchi pindi wanapojitokeza
kwenye vituo vya kusajiliwa.
Zoezi la Usajili wanachi Vitambulisho vya Taifa
linakusudiwa kumalizika mwezi Desemba mwaka huu kwa wananchi wote wenye umri wa
miaka 18 na kuendelea kuwa wamesajiliwa na kupata namba za Utambulisho wa Taifa
(NIN) wakati hatua za Uzalishaji zikiendelea sambamba na kuvigawa kwa wananchi.
Comments
Post a Comment