- Get link
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- Other Apps
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza na waandishi wa Habari Kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-Bunge mjini Dodoma (hawapo pichani) kuhusu hatua ya Serikali ya kuanza kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa Umma, kiasi cha shilingi bilioni 43.39 kuanzia Februari 10, 2018. Kushoto ni Kamishna Msaidizi-Bajeti, Bw. Emmanuel Tutuba na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Utawala) Bi. Susan Mkapa (Picha-Wizara ya Fedha na Mipango)
MAELEZO YA MHE. DKT. PHILIP ISDOR MPANGO KWENYE VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MALIPO YA MADAI YA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA KWA WATUMISHI
WA UMMA
Ndugu Wawakilishi wa vyombo vya habari, nimewaiteni leo hii ili niwape taarifa fupi kuhusu malipo ya madai ya
malimbikizo ya mishahara kwa Watumimishi wa umma waliokuwa na madai ili muweze
kuufikishia umma wa Watanzania.
Serikali kupitia mfumo wa taarifa za kiutumishi na
mishahara (Human Capital Management Information System – HCMIS) kufikia tarehe
01 Julai 2017 ilikuwa na madai ya malimbikizo ya mishahara yenye jumla ya
shilingi 127,605,128,872.81 kwa watumishi 82,111 Wakiwemo walimu 53,925
waliokuwa wanadai shilingi 53,940,514,677.23
sawa na asilimia 42.27 ya madai yote,
na wasiokuwa walimu 28,186 waliokuwa wanadai jumla ya shilingi
73,664,614,195.58 sawa na asilimia 57.73 ya madai yote. Madai haya yalikuwa ya
muda mrefu mengine yakiwa ya kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2017
Madai haya yalijumuisha mishahara isiyolipwa,
tofauti ya mishahara kutokana na kukaimu na nyongeza za mishahara zilizotokana
na kupandishwa vyeo na kuchelewa kurekebishiwa mishahara.
MATOKEO YA UHAKIKI
WA MADAI YA SHILINGI BILIONI 127,605,128,872.81 KWA WATUMISHI 82,111
a)
Madai ya watumishi 27,389 kati 82,111 yenye jumla ya shilingi 43,393,976,807.23
ikiwa ni asilimia 34 ya madai
yote ya shilingi bilioni 127,605,128,872.81 yaliyohakikiwa yameonekana ni sahihi na yanastahili kulipwa
bila marekebisho.
b)
Madai yanayostahili kulipwa
yanajumuisha shilingi bilioni 16.25
kwa walimu 15,919 na shilingi bilioni
27.15 kwa watumishi wasiokuwa
walimu 11,470
c)
Madai yote yaliyoonekana kuwa sahihi ya shilingi bilioni
43.39 yatalipwa pamoja na mshahara wa mwezi Februari 2018 kwa mkupuo mmoja. Malipo ya Madai
haya ambayo mengine yana zaidi ya miaka kumi majina ya walipwaji wote
yatatangazwa kwenye magazeti kuanzia kesho tarehe 10 Februari, 2018.
Kwa matokeo hayo ya uhakiki, mazoezi
yaliyofanyika likiwemo zoezi la
kuwaondoa kwenye Mfumo wa malipo ya mshahara (“payroll”) watumishi hewa, vyeti
feki na wasio kuwa na sifa na uhakiki wa
madai ya malimbikizo ya mishahara uliofanyika limeweza kuokoa jumla ya shilingi
bilioni 84.22 ambazo ni sawa na
asilimia 66 ya madai yote ya malimbikizo ya awali ya shilingi bilioni 127.61 yaliyokuwa kwenye mfumo ambazo bila
zoezi la uhakiki kufanyika zingelipwa
wakati zilikuwa hazistahili kulipwa.
Serikali itaendelea kulipa madai ya
watumishi kadiri yanavyojitokeza ili kuondokana na malimbikizo ya aina hii
ambayo yanaweza kuisababishia Serikali hasara kwa kulipa madai yasiyostahili.
Asanteni kwa kunisikiliza
Comments
Post a Comment