Featured Post

SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA MFUMO WAKE WA UTOAJI DAWA

 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto, Dr Faustine Ndungulile akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano  Unaojadili Namna na Mbinu za kutokomeza Uzalishaji na usambazaji wa  Dawa bandia na zisizo na Viwango katika  Masoko ya nchi za  Afrika.

Na Mwandishi Wetu
Serikali imesisitiza kwamba itaendelea kuimarisha mifumo yake ya utoaji huduma za dawa kutokana na ukweli kwamba baadhi ya dawa zinatumika kwa wanyama na binadamu na kuleta usugu wa ugonjwa husika kwa mgonjwa na
 gharama kubwa kwa taifa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na watoto,Dr Faustine Ndugulile wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa siku nne wa Jukwaa la kudhibiti usambazaji na uzalishaji wa bidhaa za madawa Afrika ambapo nchi 18 zipo nchini kujadili namna bora ya kudhibiti madawa yasiyo na viwango katika soko ili kuimarisha na ustawisha afya za wananchi wake.

“Tanzania ni moja ya nchini iliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa katika udhibiti wa dawa feki kwa Afrika nzima na mamlaka ya dawa na vipodozi nchini ina maabara za kisasa na watalaamu wa kutosha wa kuweza kufanya ukaguzi wenye ubora na viwango vya kimataifa,” amesema Ndungulile

Ameongeza kwamba Tanzania imeweza kujitosheleza kwa dawa za kutosha na zenye viwango vya kimataifa na changamoto kubwa ilikuwa na kudhibiti dawa zinazoingia kwa njia ya panya ambapo tayari mamlaka husika wameshafungua ofisi za kanda ambazo zimefanya kazi kubwa kupunguza mianya ya dawa zinazoingia kwa njia ya panya.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bi Agnes Kijo amefafanua kwamba wataalamu kutoka nchini za Cameron, Ivori Coasti, Mali, Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Mauritius, Senegal, Ethiopia, Sudan, Guinea, Sierra Leone, Uganda, Malawi, Zambia, Zimbabwe na Afrika kusini watakutana kwa siku nne ili kuja na mpango kabambe wa kudhibiti dawa bandia.

“katika mkutano huu jambo kuu litakuwa na kwa namna ngani tunaweza kudhibiti dawa bandia kwenye masoko na kuhakikisha kwamba wazalishaji pia wanatoa dawa zenye ubora unaokubalika katika soko,” amesema  Kijo.

Kijo ameongeza kwamba TFDA kwa sasa ina maabara 24 nchini nzima zenye vifaa vya kisasa vya kufanya ukaguzi nchini nzima na ofisi saba za kikanda ambazo zina wataalamu wa kutosha kuweza  kuhudumia sehemu za mikoani.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto, Dr Faustine Ndungulile, akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa Habari juu ya Umuhimu wa Mkutano huo ambao umekutanisha nchi 18 kutoka bara la Afrika huku Tanzania ikiwa Mwenyeji.
Kaimu  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini(TFDA), Agnes Kijo akizungumza jambo juu ya Mkutano huo kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto, Dr Faustine Ndungulile  kufungua MKutano huo.
 Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Afrika(NEPAD),Magreth Ndomondo akielezea umuhimu wa kuwa na chombo cha pamoja cha kudhibiti na kuhakiki Usambazajina Matumizi ya Dawa Bandia na Zisizo na Viango Barani Afrika
 Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la USP, Emily Konie akieleza namna shirika lake linavufadhili mpango wa udhibiti wa Dawa Bandia na Zisizo na Viwango Barani Afrika.
 Washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa kutengeneza Mkakati wa pamoja wa kudhibiti na kutokomeza  usambazaji na matumizi wa Dawa Bandia
 Washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa kutengeneza Mkakati wa pamoja wa kudhibiti na kutokomeza  usambazaji na matumizi wa Dawa Bandia
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto, Dr Faustine Ndungulile, akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa kutengeneza Mkakati wa pamoja wa kudhibiti na kutokomeza  usambazaji na matumizi wa Dawa Bandia 

Comments