- Get link
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- Other Apps
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Mafunzo
Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani. Wa Pili kushoto
anayevuta utepe ni Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mafunzo kutoka tume Kuu
ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian na wa kwanza kushoto anayepiga
makofi ni Balozi wa China hapa nchini Wang Ke.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa
Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya kufungua Kituo hicho cha
Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa
Mafunzo kutoka tume Kuu ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian mara baada
ya ufunguzi wa kituo hicho ambacho kimejengwa kwa msaada kutoka Jeshi la Ukombozi
la watu wa China.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga
Taifa Dkt. Husein Mwinyi wakati alipokuwa akiandika jambo katika hotuba yake.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi mara baada ya kufungua
Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa China hapa nchini, Wang Ke mara
baada ya kukifungua kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi
wa Mafunzo kutoka Tume Kuu ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian mara
baada ya kukifungua kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati alipokuwa
akizungumza na Mbunge wa Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa, Mbunge wa Chalinze
Ridhiwan Kikwete pamoja na Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo mara
baada ya kufungua kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mapinga(hawaonekani
pichani) waliokuwa wakiwasilisha kero mbalimbali za ardhi wakati alipokuwa
akirejea jijini jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungua kituo hicho cha
Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga mkoani Pwani.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makomandoo
wa JWTZ ambao walishiriki katika mazoezi ya Kijeshi kabla ya ufunguzi wa kituo
hicho.
Kikundi cha Ngoma za asili cha Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa
Tanzania kikitumbuiza wakati wa sherehe za ufunguzi wa kituo hicho cha Mafunzo
maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga mkoani Pwani. PICHA NA IKULU
Comments
Post a Comment