Featured Post

MGEJA: TAIFA LIMUENZI MZEE KINGUNGE NGOMBALE KWA MAZURI YAKE


Na Hastin Liumba,Kahama
MWENYEKITI wa Tanzania Mzalendo foundation inayoshughulikia haki na utawala bora, Khamis Mgeja amesema taasisi yake inaungana na watanzania wote kwa kuondokewa na mwanasiasa mkongwe Mzee Komredi Kingunge Ngombale Mwiru ambaye katika maisha yake alilitumikia taifa kwa utumishi uliotukuka.


Mgeja alisema hayo wakati akiwa kwenye mapunziko ya kilimo wakati alipokutana na waandishi wa habari wilayani Kahama mkoani Shinyanga na ambapo alisema msiba huo ni mzito kwa kiongozi huyo.
Mgeja alisema ni vyema watanzania kwa kushirikiana na serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk JohnMagufuli kumuenzi na kumpa heshima yake stahiki kama kiongozi aliyelitumikia taifa kwa uadilifu mkubwa.
Mwenyekiti huyo alisema yeye binafsi na taasisi yake atamkumbuka mzee Kingunge na kumuenzi kwamba jinsi ambavyo alikuwa akiliamini suala lolote linalogusa maslahi ya ya taifa na maslahi ya wananchi alikuwa akitetea kwa nguvu zake zote bila kuyumba au kuyumbishwa na mtu yoyote.
Mgeja alisema na kuongeza kuwa Mzee Kingunge Ngombale Mwiru alikuwa mkweli,siyo muongo ,mpiga majungu,mropokaji,mfitini na muwazi na mwenye kujenga hoja,na alikuwa mfano wa kuigwa na alikuwa ni mwanasiasa ambaye ni  wachache na  wa aina yake nchini.
Alisema kutokana na hali hiyo taifa limeondokewa na mtu muhimu katika kipindi hiki.
Aidha mwenyekiti huyo aliongeza kuwa katika msiba wengi waliopita katika mikono ya Mzee Kinginge Ngombale Mwiru katika nasaha na ushauri wake inapaswa sasa kuyaendeleza yale mazuri na mema aliyotuachia kwa kudumisha upendo,mshikamano kwa maslahi mapana ya taifa.
‘Nawapongeza viongozi wote na serikali na vyama mbalimbali bila kujali itikadi za dini zao kwani wamekuwa ni mfano wa Tanzania tuliyoachiawa na baba wa Taifa Hayati mwalimu Julias Nyerere.’aliongeza.
Alisema ni matumani na maombi yake mzee huyo aenziwe kitaifa kwa sababu ya uzalendo hauna itikadi ni Tanzania na watanzania kwanza.

Comments