Featured Post

MAKAMU WA RAIS KATIKA SIKU YA PILI WILAYA YA KILOLO MKOANI IRINGA

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Juma Abdallah akisoma taarifa ya wilaya yake mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati ziara ya Makamu wa Rais wilayani Kilolo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya Wilaya ya Kilolo ikiwa siku ya pili ya ziara yake mkoani Iringa, wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe. Venance Mwamoto (kulia) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Bw. Salim Abri Asas. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe. Venance Mwamoto akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la Utawala la Shule ya Sekondari Kilolo ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka mkoa wa Iringa Ndugu Salim Abri Asas akihutubia wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa jengo la Utawala la shule ya Sekondari Kilolo ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa jengo la Utawala la Shule ya Sekondari ya Kilolo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Iringa B. Amina Masenza wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la Utawala la shule ya sekondari ya Kilolo mkoani Iringa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)​

Comments