Featured Post

CCM MKOA WA IRINGA YATOA MSAADA WA BATI 300 NA MIFUKO YA SARUJI 500 KWA HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

Katibu wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Iringa Christopher Magala akizungumzia utekelezaji wa ila ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa.

 Na hii ni baadhi ya mifuko ya saruji na bati walizopewa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Manispaa ya Iringa Said Rubeya akifanya kazi kwa vitendo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo 
 Mwenyekiti wa umoja wa vijana Mkoa wa Iringa Kenani kihongosi akifanya kazi kwa vitendo
 Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Ritta Kabati akifanya kazi kwa vitendo 

Na Fredy Mgunda, Iringa
Chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa kimeanzimisha miaka arobain na moja (41) kwa kutoa msaada wa bati mia tatu (300) na mifuko ya saruji mia tano (500) kwa halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa ajili ya kusaidia ukarabati na ujenzi kwenye shule zenye mahitaji hayo kwa kufanya kazi za kimaendeleo 
 
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Katibu wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Iringa Christopher Magala alisema kuwa wameamua kutoa msaada kwa kutimiza malengo ya ilani ya chama cha mapinduzi  ya mwaka 2015 hadi 2020 kwa kuwatumikia wananchi waliowaweka madarakani hivyo kufanya ni sehemu ya kazi za chama.

“Tunachokifanya hii leo ni kuendelea kuonyesha wananchi waliotuweka madarakani jinsi gani tunavyofanya kazi kwa mjibu wa ilani yetu kama mwenyekiti wa chama Dr John Pombe Magufuli anavyotekeleza vizuri ilani yetu” alisema Magala

Magala alisema kuwa halmashauri ya manispaa ya Iringa imekuwa kama yatima kimaendeleo kutokana na utendaji kazi wa viongozi wanayoingoza halmashauri hivyo chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa kimeamua kuanza kufanya kazi za kimaendeleo kwa wananchi.

“Leo hii hakuna kitu kipya ambacho kimefanya na halmashauri ya Iringa ndio maana tumeingia kazini kufanya kazi kwa nguvu zetu zote hivyo tutawatumikia wananchi ipasavyo na kuhakikisha manispaa inasonga mbele kimaendeleo” alisema Magala

Magala alisema kuwa wameamua kukabidhi misaada hiyo sambamba na kufanya kazi katika shule ya sekondari ya Mawelewele iliyopo kata ya Mwangata kama mfano wa kuikwa kwa wananchi wa kata hiyo sambamba na wanafunzi na viongozi wengine kufanya kazi kwa vitendo na sio kukaa tu maofisini.

“Leo tunakabidhi kama mfano tu wa msaada wetu hapa shuleni tunatoa bati mia hamsini na mifuko ya saruji sitini kwa lengo la kusaidia kumalizika kwa ujenzi huu ambao unaendelea hii leo hivyo naomba uupokee msaada huu ambao najua kwa kiasi furani utachangia maendeleo ya shule hii” alisema Magala

Aidha Magala aliwataka walimu wa shule hiyo kufundisha kwa kuhudi na maarifa ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi wa shule hiyo kwa kuwa serikali inatoa elimu bure bila malipo na kufanikisha kila mtoa apate elimu inayostali.

“Naombeni na sitaki kusikia kuna mtoto amefukuzwa shule kwa kukosa ada wala michango yoyote ile hapo mtanijua mimi nani na jinsi gani navyosimamia ilani ya chama changu hivyo naomba mfanye majukumu yenu kama mnavyotakiwa kufanya” alisema Magala

Magala aliwataka viongozi wote wa mkoa,wilaya, kata hadi tawi kuhakikisha wanafanya kazi vuizuri kwa kusimamia ilani ya chama cha mapinduzi ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ambao wamewaka madarakani.

Baada ya kupokea msaada huo mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alikishukuru chama cham mapinduzi mkoa wa Iringa kwa kutoa msaada huo ambazo utasaidia kutatua matatizo ya miundimbinu ya shule za manispaa ya Iringa ambazo zipo taabani kabisa.

“Kazi mnayoifanya kweli ilitakiwa kufanywa na serikali ya halmashauri ya manispaa ya Iringa lakini imeshindwa hivyo naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa viongozi wangu wote CCM mkoa wa Iringa kwa kazi kubwa mnayoifanya kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo” alisema Kasesela

Kasesela aliongeza kuwa kuwepo kwa upinzani ndani ya halmashuri ya manispaa ya Iringa kunarudisha nyuma maendeleo ya wananchi kwa kuwa wapinzani hawafanyika kazi kama inavyostahili hivyo tunaomba viongozi wa chama mtusaidie msaada wa kutuletea maendeleo.

“Halmashauri ya manispaa ya Iringa ni yatima hivyo tunaomba chama cha mapinduzi kupitia viongozi wangu mtusaidie kufanya shughuli za kimaendeleo msiishie leo tu maanakuna vitu vingi bado havijakaa sawa” alisema Kasesela

Kasesela akatoa agizo kwa kiongozi yeyoto Yule atakayetumia vibaya msaada huo ulitolewa na chama cha mapinduzi atakula naye sahani moja hadi atajuta kwa kwanini ametumia vibaya msaada huo.

Comments