Featured Post

BULYANHULU YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI 75,649,524 KWA HALMASHAURI YA NYANG’HWALE

Meneja Mkuu wa Migodi wa  Bulyanhulu Benedict Busunzu akikabidhi hundi ya milioni 75,649,524  kwa Mkuu wa wilaya ya   Nyangh’hwale  Hamim Gweyama  kwa ajili ya malipo ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya wilaya ya hiyo katika kipindi cha mwezi Julai hadi Disemba 2017.

Meneja Mkuu wa Mgodi  wa Bulyanhulu Benedict Busunzu akizungumza na madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale  ambapo alisema Acacia itaendelea kushirikiana na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi .

Meneja Mkuu wa Migodi wa Bulyanhulu Benedict Busunzu akifurahia pamoja na wafanyakazi wa Bulyanhulu baada ya kukabidhi hundi kwa halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale.


Na,Joel Maduka, Nyang'hwale
Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu Acacia kupitia mgodi  wake  wa Bulyanhulu imekabidhi hundi ya shilingi milioni  75,649,524 kwa halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita kwa ajili ya malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha Mwezi Julai hadi Disemba mwaka 2017.

Akikabidhi mfano wa hundi hiyo  mbele ya madiwani wa halmashauri hiyo Meneja  wa  Mgodi  huo,  Benedict  Busunzu,  alisema  kawaida  mgodi  huo hutoa  ushuru  kwa  Wilaya  mbili  ya   Msalala  na  Nyangh’hwale  kwa  ajili  ya  miradi  ya  maendeleo.

Aidha  alitaja  moja  ya miradi  mingine  ambayo  mgodi  huo  umesaidia  Wilayani  humo  ni  pamoja  na  mradi  wa  mkubwa  wa  kusambaza   maji kwa  wakazi  150,000 wilayani  humo,   wenye  gharama  ya  Shilingi  Bilioni 4.5  ambao  unatarajiwa  kukamilika  mwishoni  mwa  mwaka  huu.

Aidha kwa upande wake Katibu tawala wa Mkoa wa Geita, Celestine Gesimba amewataka madiwani    na watendaji  wa  halmashauri ya hiyo    kuepuka   kutumia  fedha  zinazotolewa  na wadau  mbali mbali    kwa ajili  ya  miradi ya maendeleo  kwa  kulipana  posho  za  vikao,   badala  yake  zote  zitumike  katika miradi  kwa  manufaa  ya  ustawi  wa wakazi  wa Wilaya  hiyo.

“Ninapenda  kuwaonya  viongozi  na watendaji    ambao mpo hapa Nyangh’wale  kuwa  tusitumie hizi  fedha  kwa  ajili  ya kulipana  posho  za  vikao  badala  yake  zote  zietumike  katika  miradi  ya  maendeleo  kwa  jinsi  mtakavyoainisha,”alisema Gesimba.

  Aidha Mkurugenzi  wa  Wilaya  ya  hiyo,  Carlos  Gwamagobe,  pamoja na kushukuru mgodi  mgodi  huo  kwa kuwapatia  fedha  hizo alisema ushuru wa huduma ambayo walikuwa wakipata hapo awali  umeshuka kwani kwa  kiasi kikubwa kwani walikuwa wakipokea milioni mia nne kwa miezi sita .


“Tuna  imani  kuwa  mgodi  huu ukianza  shughuli  zake  kama  ilivyokuwa  awali   hata  ushuru  wa  huduma  utaongezeka  kwani awali  tulikuwa  tukipatiwa  kiasi  cha  Shilingi  Milioni  225   lakini  tangu  kuibuka  kwa  sakata  la  Makinikia,  ushuru  nao  umepungua  mara  mbili  ya  zile  za  awali,”alisema Gwamagobe.

Comments