Featured Post

WAZIRI JAFO ATAKA WAUGUZI WAPATIWE MAFUNZO YA DAWA ZA USINGIZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua mradi wa maji wa Kijiji cha Mima.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo
akipata maelezo ya ujenzi wa majengo kwa teknolojia ya ‘Prefabricated’


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Mpwapwa George Lubeleje wakipata maelezo kutoka kwa mkandarasi anayejenga kituo cha Afya Mima wilayani Mpwapwa.

Ujenzi wa jengo la Maabara unavyoendelea katika Kituo cha Afya Mima wilayani Mpwapwa kwa kutumia teknolojia ya ‘prefabricated’.
Moja ya kutuo cha afya kinachoboreshwa hapa nchini katika mpango kabambe wa uboreshaji wa vituo vya afya.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mima.
........................................................................................
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amezitaka Ofisi za wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya nchini kuteua wauguzi kati ya wawili hadi wanne kwa kuwapeleka kwenye mafunzo maalum ya dawa za usingizi ili waweze kutoa huduma hiyo wakati wa upasuaji kwenye vituo vya afya.
Waziri Jafo ametoa maelekezo hayo ya serikali leo alipokuwa anakagua uboreshaji wa kituo cha Afya Mima kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Amesema mafunzo hayo yawe ya muda mfupi na muda mrefu ili kujiweka tayari katika kuwahudumia wananchi ipasavyo kwenye huduma za upasuaji kutokana na serikali ya awamu ya tano kwasasa inaboresha vituo vya afya nchini kwa kuvijengea vyumba vya upasuaji na miundombinu mbalimbali.
"Wakati tunaendelea kuboresha vituo vya afya hapa nchini niwatake wakurungezi wa halmashauri na waganga wakuu wa wilaya zote kuwawezesha wauguzi wenu katika fani za dawa za usingizi kwa kutumia chuo cha Muhimbili, KCMC, na vyuo vingine hapa nchini ili kazi hii ya ujenzi inapokamilika na vifaa vya upasuaji vitakapoweka ninyi muwe mmejiandaa na sio kubweteka mnasubiri kila jambo muelekezwe,”Amesema Jafo
Ameongeza “Nataka mujiongeze kwani japo serikali tunaendelea kuajiri madaktari na wauguzi lakini nyinyi mnapaswa pia kujiongeza kwenye hili ili wananchi wetu waweze kupata huduma bora,".
Katika ziara yake wilayani Mpwapwa, Waziri Jafo amefanikiwa kukagua miradi mingine ya ujenzi ikiwemo barabara za lami zinazojengwa na Wakala wa barabara mijini na vijijini (Tarura) katika mji wa Mpwapwa na mradi wa maji wa kijiji cha Mima.

Comments