Featured Post

WAITAKA SERIKALI KUMALIZA KAMATA KAMATA YA WANANCHI INAYOFANYWA NA ASKARI WA MKUNGUNERO

Na Woinde Shizza, Kondoa

Wananchi wa vijiji 11 kwenye kata sita wilayani Kondoa wameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kumaliza migogoro inayotokea kati yao na Askari wa Pori la Akiba la mkungunero kwani wananchi hao wamekuwa wakibambikiwa kesi za  mara kwa mara na Askari hao na kugeuzwa miradi kwa madai ya mifugo.

Licha ya mda mrefu kupita na kutulia kwa migogoro pembezoni mwa pori la akiba la Mkungunero na Wananchi wa vijiji 11 bado kumekuwa na kamata kamata ya wananchi na kujikuta wanafunguliwa kesi ambapo mifugo zaidi ya 146 inashikiliwa na Askari wa wanyapori ndani ya hifadhi hiyo huku wananchi watatu wakishikiliwa tokea demember 26 mwaka jana na kesi yao ipo mahakamani hadi december  5 mwezi huu.


Wakizungumza kwa niaba ya Wananchi hao Diwani wa Kata ya Itaswi Issa Chobu alisema kuwa licha ya mgororo huo kuwepo kwa mda mrefu lakini Tatizo kubwa ni Serikali kushindwa kufuatilia ripoti ya tume iliyoundwa waziri mkuu ya mwaka 2012 ili wananchi waliohamishwa ndani ya hifadhi wakati huo walipwe fidia zao.


Alisema kuwa licha ya wananchi kukaa na viongozi wa Pori hilo la Akiba na kuona wanatatatuaje matatizo ya unyweshaji wa maji mifugo na wananchi kutumia maji hayo kwa matumizi yao bado tatizo kubwa kwenye mgogoro huo ni huduma bora ya maji na hilo litaondoa tatizo la mifugo na wananchi kuingia ndani ya hifadhi .

“Mimi kama mwakilishi wa wananchi naiomba serikali kuangalia upya ripoti ya tume iliyoundwa na waziri mkuu pinda wakati huo naona hii itasaidia kuondoa dhana nzima ya migogoro na kurudisha uhifadhi shirikishi kwa maendeleo ya taifa na uhifadhi.”alisema Chobu
Nae Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kutish Adamu Ally amesema kuwa wao kama majirani wema wa hifadhi waliomba kunywesha mifugo kwenye mto unaoanzia milima ya haubi na kupita mita 120 ndani ya hifadhi karibu na kitongoji changu katika kikao chao na viongozi wa pori hilo la Akiba mwezi wa Tano mwaka jana na kukubaliwa lakini kwa kipindi cha kiangazi lakini cha kushangaza kila wakipeleka mifugo kunyesha wamekuwa wakikamatwa na kutozwa kiasi cha 50,000  kwa kichwa cha mfugo.

Alisema kuwa wamekuwa wakitoa malalamiko yao mara kwa mara lakini wananchi wameendelea kukamatwa na kufunguliwa kesi kama wenzao watatu wamekamatwa toka desember 26 na kufikishwa mahakamani licha ya wao kutokuwepo  wakati mifugo inakamatwa.

Juhudi za kumpata Meneja wa Pori hilo la Akiba kwa njia ya Simu zinaendelea licha ya kuwa alikuwa hapatikani hewani ili aweze kujibu tuhuma hizo zilizoelekezwa kwenye uongozi na watumishi wa Poti hilo la Akiba la Mkungunero

Gazeti hili limefika kwenye eneo la tukio na kujionea na kusikiliza pande mbali mbali za serikali za vijiji hiyo na kata na kugundua kama serikali itafuata ushauri huu basi mgogoro huo utakuwa Historia,Moja Kuanzisha(WMA) Uhifadhi shirikishi,Pili uwepo wa Ujirani Mwema,na Tatu  kuisaidia huduma za kijamii kwa mapato inayotokana na uwindaji kwenye hifadhi hizo za Akiba.

Comments