Featured Post

MBUNGE MGIMWA ATUMIA SHS. 119.2 MILIONI KUJENGA MADARASA YA SHULE ZA MSINGI, ZAHANATI NA NYUMBA ZA WAFANYAKAZI KATIKA KIJIJI KIBENGU


 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini, Mahamuod Mgimwa akizungumza na wananchi katika moja ya shule ambayo inahitajika kujengewa vyumba viwili ya madarasa na kukarabati vyumba vingine vitatu kwa gharama za wananchi na mbunge mwenyewe akichangia kwa asilimia kubwa kuboresha maendeleo ya sekta ya elimu kwa wananchi na wanafunzi wa jimbo hilo
 Mbunge wa jimbo la Mufindi KaskaziniMahamuod Mgimwa akizungumza mmoja ya walimu pamoja viongozi kutoka kwenye ofisi yake ya mbunge ambao alikuwa ameongoza nao katika kukagua na kutatua changamoto za wananchi kwenye kata ya Kibengu
 Mbunge wa jimbo la Mufindi KaskaziniMahamuod Mgimwa akitoa mfano wa kufanya kazi kwenye ujenzi wa vyumba vitatu vya shule ya msingi Kibengu ambako nako wananchi wamechangia nguvu zao
 Katibu wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM wilaya ya Mufindi akiwa na katibu wa mbunge idara ya uhamasishaji na michezo Lwimbo nao wakijumika na wananchi katika ujenzi wa shule ya msingi Kibengu
 Mbunge wa jimbo la Mufindi KaskaziniMahamuod Mgimwa akizungumza na viongozi katika eneo ambalo vyumba vitatu vya madarasa vinajengwa
 Mbunge wa jimbo la Mufindi KaskaziniMahamuod Mgimwa akizungumza kwenye eneo ambalo ofisi ya kijiji inajengwa ajili ya kurahisisha kutoa huduma kwa wananchi
Mbunge wa jimbo la Mufindi KaskaziniMahamuod Mgimwa akiwa na diwani wa kata ya Kibengu Zakayo Kilyenyi sambamba na katibu wa mbunge idara ya uhamasishaji na michezo Lwimbo

 Na Fredy Mgunda,Mufindi Kaskazini.

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kwa kushirikiana na wananchi  wa kijiji cha Kibengu wametumia jumla ya shilingi milioni mia moja kumi na tisa na laki mbili (119,200,000) katika ujenzi wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kijiji hicho lengo likiwa katika kuboresha sekta ya elimu na afya kwa wananchi.

Akizungumza na wananchi katika kijiji hicho mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa alisema kuwa ameamua kuwekeza katika elimu na afya kwasababu wananchi wakifanikiwa kupata vitu hivyo viwili kwa wakati watafanya maendeleo kwa kasi kubwa kulingana na wakati uliopo na kuendana na mazingira wanayoishi.

“Hivi ndio vipaumbele vyangu kwa kijiji hiki kwa wakati huu maana nimegundua kuwa changamoto kubwa ni kuwa shule nyingi za msingi zilijengwa miaka mingi iliyopita sasa zimechakaa na sio rafiki kwa wanafunzi kuwasaidia kupata elimu bora hivyo nimeanza na hilo pamoja na kuchangia maendeleo kwa kuboresha sekta ya afya ili wananchi wakiugua waweze kutibia hapa hapa kijiji kwa kuwa nina uhakika huduma itakuwa inatolewa kwa ustadi mkubwa na yenye ubora unaotakiwa” alisema Mgimwa

Mgimwa alieleza kuwa pesa hiyo itatumika katika maeneo yafuatayo ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Kibengu utatumia gharama ya shilingi milioni thelathini (30,000,000) hadi kukamilika kwake,kuingiza umeme zahanati na kwenye nyumba za waganga imegarimu kiasi cha shilingi 1,200,000/=,ujimbaji wa kisima shilingi 2,00,000/=,ujenzi wa nyumba za walimu mbili kwa moja itagharimu kiasi cha shilingi 25,000,000/= na shule ya msingi Kibengu kutafanyika ujenzi wa madarasa matatu ambayo yatagharimu kiasi cha shilingi 21,000,000/=.

“Hizi ni gharama katika kijijicha Kibengu ambazo nimechangia na wananchi wangu hivyo napenda kuwapa habari vijiji na vitongoji vingine kwenye jimbo langu kuiga mfano wa kijiji cha Kibengu na kitongoji cha Mitanzi kwa kujituma kuleta maendeleo” alisema Mgimwa

Aidha Mgimwa alisema kuwa wananchi wa kitongoji cha Mitanzi katika kijiji cha Kibengu nao wamekuwa wakitoa ushirikiano na kufanikisha kufanya maendeleo katika maeneo yafuatayo ujenzi wa nyumba za walimu na madarasa ya shule ya msingi Mitanzi utagarimu kiasi cha shilingi milioni kumi na saba (17,000,000) uchimbaji wa kisima  shilingi 1,000,000/=, ukarabati wa madarasa mawili shilingi 17,000,000 kutona na yalivyo haribika, kuingiza umeme kwenye nyumba za walimu na madarasa shilingi 5,000,000/=

“Ukaingalia tumetumia nguvu kubwa na wananchi kufanikisha haya japo kuna maeneo bado hatujamalizia na ninauhakika tutamalizia lakini bado kunawatu wanasema eti sifanyi kazi sasa sijui wataka niwe ninawapa pesa mikononi mwao ili wajue maendeleo yapo” alisema Mgimwa

Mgimwa alimalizia kwa kuwaomba wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuendelea kumuunga mkono katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo kwa kuwa wanajinea kazi anayoifanyia hivyo wasikubali kulishwa maneno na watu wasiopenda maendeleo.

Kwa upande wake mtendaji wa kijiji cha Kibengu Dominicus Nyaulingo alimshukuru mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kwa jitihada zake za kuleta maendeleo kwa kushirikiana na wananchi na kahidi kuwa watandelea kuzitangaza kazi anazozifanya ili wananchi wote wajue anafanya kazi gani na kupunguza maneo ambayo yamekuwa yakisemwa bila kuwa na ushaidi juu ya utendaji wa mbunge huyo.

“Kweli kabisa mbunge wetu amekuwa akifanya kazi kubwa sana ila sisi tumekuwa hatuzisemi kazi za mbunge kwa wananchi hivyo kuchochea chuku baina ya wananchi na mbunge hivyo kuanzia leo nitakuwa ninazisemea kazi za mbunge kila kwenye mkutano wa kijiji” alisema Nyaulingo

Comments