Featured Post

LAND TENURE SUPPORT PROGRAMU YADHAMIRIA KUMALIZA MIGOGO YA ARDHI MKOANI MOROGORO

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi, Doroth Mwanyika amefanya ziara kwenye Wilaya za Kilombero, Malinyi na Ulanga ni wilaya tatu zilizochaguliwa kutekeleza zoezi la upimaji na urasimishaji wa ardhi kwa majaribio katika mkoa wa Morogoro lengo kuu likiwa ni kupanga matumizi bora ya ardhi ili kupunguza migogoro na ugomvi  baina ya wakulima na wafugaji.
Akihutubia wananchi hao, Katibu mkuu aliwataka wanavijiji hao kutumia fursa mbalimbali zilizo sanjari na mradi wa upimaji na urasimisha ardhi ili kujiletea maendeleao katika ngazi ya familia, Kijiji na taifa kwa ujumla.
Alisema migogogo ya ardhi ni imekuwa chanzo kikubwa cha kudorora kwa maendeleo maeneo husika kutokana na muda mwingi kutumika kukashughulika kutatua migogoro hiyo na kutumia muda mchache kwenye  shughuli za maendeleao.
Katibu Mkuu pia amewashuru wananchi kwa utayari wao wa kumaliza migogoro na kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali ili kujiletea maendeleo yao na Taifa letu.  
AFISA Mipango wa Miji na Vijiji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Nickson Mjema akimpatia muhtasari Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Doroth Mwanyika kuhusu elimu na mikakati ya kuwahamasisha na kutoa elimu kwa wna Kijiji wa Nakafulu, wakati wa ziara ya Katibu huyo Wilaya ya Ulanga Mkoa wa Morogoro Januari 10 2018. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)



KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi, Doroth Mwanyika akijaliana jambo na mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Jacob Kassema wakati wa ziara yake kwenye Kijiji cha Nakafulu, Wilayani humo Mkoani Morogoro Januari 10 2018.

MPIMAJI wa Ardhi wa Land Tenure Support Programu (LTSP), Gilbert Utama akimfafanulia Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika jinsi tekiolojia ya mtandao wa simu inavyorahisha upimaji ardhi wakati wa upimaji ardhi kwenye Kijiji cha Ipunguo Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro Januari 10 2018. Kushoto (kwa katibu Mkuu) ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Jacob Kassema, Katibu Tawala, viongozi wa wizarani na watendaji wa serikali za mtaa  wa Mkoa huo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika ( wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu wa watendaji wa wizara walipowasili Mlima Ndororo na Mkoa wa Morogoro wakati wa ziara ya kikazi Januari 10, 2018.

MMOJA wa wana Kijiji cha Ipungua aliyenufaika na mradi wa Land Tenure Support Programm (LTSP), Yusta Makoto akionesha Kitambulisho chake ambacho hutumika pia na wana vijiji wengine kutambuliwa na kusajiliwa tayari kwa kupatiwa hati za umuliki wa ardhi Mkoani humo.

MMOJA wa wana Kijiji cha Ipungua aliyenufaika na mradi wa Land Tenure Support Programm (LTSP), Dastan Kaweza akionesha pia Kitambulisho chake ambacho hutumika pia na wana vijiji wengine kutambuliwa na kusajiliwa tayari kwa kupatiwa hati za umuliki wa ardhi Mkoani humo.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika (wa nne kulia) na mwenyeji wao, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Jacob Kassema wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu wa watendaji wa wizara walipowasili wilayani hapo Mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kikazi Januari 10, 2018.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika akiongea na kuwapongeza wana Kijiji cha Nakafulu baada kushiriki kwenye mkutano wa hadhara uliolenga kuwapatia elimu na hamasa ya upimaji na urasimisha ardhi katika Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro Januari 10 2018.

SEHEMU ya wananchi wa vijiji vya Signali, Sululu na Sakamaganga wilaya ya Kilombero wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Doroth Mwanyika.

SEHEMU ya wananchi wa vijiji vya Signali, Sululu na Sakamaganga wilaya ya Kilombero wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Doroth Mwanyika.


MWANA Kijiji cha Ipungua ambaye ni mmoja wa walionufaika na mradi wa Land Tenure Support Programm (LTSP), Diana Mbangayao akionesha kitambulisho chake cha kupigia kura ambacho hutumika pia na wana vijiji wengine kutambuliwa na kusajiliwa tayari kwa kupatiwa hati za umuliki wa ardhi Mkoani humo.

MPIMAJI wa Ardhi wa Land Tenure Support Programm (LTSP), Gilbert Utama akimmwonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika jinsi  mtandao wa simu inavyotumika kufanya kazi katika kupima ardhi wakati wa zoezi la upimaji ardhi kwenye Kijiji cha Ipunguo Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro Januari 10 2018. Kulia kwa Katibu Mkuu ni Mmiliki wa ardhi hiyo, Diana Mbangayao.

SEHEMU ya msafara wa Katibu Mkuu huyo na watendaji wa serikali wakitembelea miradi mbalimbali ya Ardhi katika Kijiji cha Idunda Wilaya ya Ulanga Mkoa wa Morogoro.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika akiongea na kuwapongeza wana Kijiji cha Nakafulu baada kushiriki kwenye mkutano wa hadhara uliolenga kuwapatia elimu na hamasa ya upimaji na urasimisha ardhi katika Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro Januari 10 2018.

WANAKIJIJI cha Nakafulu wakimsikiliza katibu Mkuu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika alipowasili kijijini hapo baada ya kushiriki kwenye mkutano wa hadhara uliolenga kuwapatia elimu na hamasa ya upimaji na urasimisha ardhi katika Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro Januari 10 2018.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika akipata maelezo ya alama maalum zinazotumiwa kwenye mradi wa Land Tenure Support Programm (LTSP) kutoka kwa watendaji wa serikali wa wizara hiyo alipotembelea miradi mbalimbali ya Ardhi katika Wilaya ya Ulanga Mkoa wa Morogoro.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika akipata maelezo ya eneo la makaburi kwenye kijiji cha Idunda kutoka kwa watendaji wa serikali wa wizara hiyo alipotembelea miradi mbalimbali ya Ardhi katika Wilaya ya Ulanga Mkoa wa Morogoro.

Comments