- Get link
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- Other Apps
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye.
TAARIFA KWA UMMA
UKAGUZI
WA KINGA NA TAHADHARI DHIDI YA MOTO
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
limeundwa na linatekeleza majukumu yake chini ya Sheria ya Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji namba 14 ya mwaka 2007 (Fire and Rescue Force Act No. 14 of 2007). Majukumu makubwa ya Jeshi hili ni kuokoa Maisha na Mali katika
majanga yatokanayo na moto, mafuriko, tetemeko la ardhi, ajali za barabarani
pamoja na majanga mengine.
Sambamba na majukumu hayo Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji linafanya ukaguzi kwenye vyombo vya usafiri na
usafirishaji, na kutoa ushauri uwekaji wa vifaa vya kinga na tahadhari. Ukaguzi
huu unafanyika kwa mujibu wa sheria namba 14 ya mwaka 2007 ikisomwa pamoja na
kanuni ya Vyeti na Usalama wa moto Mwaka 2008 na marekebisho ya mwaka 2014 (Fire and Rescue Force Safety
Inspections and Certificates Regulations of 2008 GN.106 and its Amendment GN 63
of 2014.) Pamoja na kanuni ya tahadhari dhidi ya moto kwenye majengo ya
mwaka 2015 (Fire and Rescue Force Fire Safety Precaution in Building
Regulations of 2015 GN 516.)
Kwa kuzingatia majukumu hayo
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linajulisha umma kuwa, halifanyi biashara ya kuuza
vifaa vya kuzimia moto wala kuvifanyia matengenezo (service) vifaa hivyo pamoja na mifumo ya kinga na tahadhari dhidi
ya moto. Bali Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linasimamia na kuhakiki ufungwaji wa
vifaa hivyo.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
linatoa rai kwa wamiliki wa majengo na vyombo vya usafiri na usafirishaji,
wafanyabiashara na wananchi wote kuhakikisha wananunua au kufanyia matengenezo (service) vifaa na mifumo ya kinga na
tahadhari dhidi ya moto kwa Mawakala waliosajiliwa kuuza vifaa vya Zimamoto (Fire
Dealers) kwa mujibu wa sheria ya Jeshi.
Imetolewa na;
Ofisi ya Habari na
Elimu kwa Umma
Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji
03 Januari, 2018
Comments
Post a Comment