Featured Post

MBUNGE RITTA KABATI AWAJENGEA KIVUKO WALEMAVU MKOANI IRINGA


 Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akizungumza wakati wa kukabidhi kivuko hicho kwa chama cha walemavu mkoa wa Iringa.
 Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akikata upete  wa kuashiria kivuko kimezinduliwa rasmi
 Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na mmoja wa walemavu akipita katika kivuko hicho
Mmoja wa watu wenye ulemavu akipita kwenye kivuko hicho kuelekea kwenye ofisi zao za chama cha walemavu mkoani Iringa.

Na Fredy Mgunda, Iringa

Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amewajengea kivuko walemavu katika ofisi yao kwa lengo la kuwarahisishia kufika ofisni hapo.

Akizungumza wakati wa kuzindua kivuko hicho Mb Kabati alisema kuwa lengo la kuwasaidia mara kwa mara watu wenye ulemavu ni kutokana kuwa kila mtu ni mlemavu mtarajiwa.

“Unajua hakuna mtu aijua kesho yake hivyo usipowajali walemavu leo hata wewe kesho ukiwa mlemavu watu hawata wajali mimi binafsi nawajali sana walemavu kwa kuwa nao ni binadamu kama binadamu wengine” alisema Kabati

Kabati alisema kuwa ametumia gharama zake binafsi kujenga kivuko hicho ambacho kitakuwa msaada kwa watu wote wenye ulemavu kufika ofisini kwa urahisi kabisa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

“Saizi naona mambo yatakuwa safi maana kila kitu naona kimetuwa bora na mafundi wamejenga vizuri na kivuko hiki naona ni imara sananaombeni na nyinyi mkitunze sana hiki kivuko” alisema Kabati

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama cha walemavu mkoa wa Iringa (CHAWATA) Rukia Makweta alimshukuru mbunge huyo kwa kuwajengea kivuko hicho maana kimewaondolea adhabu ya kudondoka dondoka wakati wanaingia ofisini kutokana na ubovu uliokuwepo.

“Unajua hiki kivuko kilikuwa na mashimo mengi hivyo ilikuwa kazi kubwa kufika ofisini maana walemavu wengi walikuwa wanaanguka sana katika eneo hili hivyo kujengwa kwa kivuko hiki walemavu wengi watakuwa wanakuja ofisini bila woga wa kuanguka” alisema Makweta

Comments