- Get link
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- Other Apps
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini Blog
WAFUGAJI wa sungura wanaweza kuwa wameshuhudia wakati
mwingine macho ya sungura wao yakionekana kutokeza juu zaidi au kuwa pembeni na
kushindwa kuzunguka kama ilivyo kawaida.
Tatizo hili kitaalam linaitwa Exophthalmos ambapo macho ya sungura huwa yako pembeni ya mfumo
wake kutokana na ugonjwa au uvimbe nyuma ya jicho.
Jicho linakuwa limesukumwa kwa mbele na nje ya soketi yake,
lakini inategemea na mahali uvimbe ulipo, kwani jicho pia linaweza kusukumwa
hata kwa nyuma ikiwa uvimbe uko mbele.
Sungura wako, hasa wa jamii ya Dwarf na Lop, pamoja na wale
wa kawaida walio katika umri wa kati wanaweza kupatwa na tatizo hili kutokana
na matatizo ya msingi ya meno au ya kinywa.
Dalili na Aina
Aina za magonjwa haya ya njia ya mzunguko wa macho (orbital disease) ni pamoja na:
* Jicho kukaa pembeni
(malpositioned eye) — husababishwa na
mabadiliko ya ukubwa (kupungua au kuongezeka) kwa vitu kwenye jicho, au kuvimba
kwa misuli ya juu ya jicho (extraocular
muscle)
* Kuvimba kwa jicho (Enophthalmos) — husababishwa na
kukosekana kwa ukubwa wa nafasi ya kuzunguka kwa jicho au nafasi hiyo kuvimba
kwa juu na kulisogeza jicho mbele
* Makengeza (Strabismus) — mzunguko usio wa kawaida
wa macho – husababishwa na mwenendo mbovu wa misuli.
Dalili za matatizo haya ya mzunguko wa macho zinaweza
kutofautiana lakini zinahusisha magonjwa ya meno, kurefuka kwa meno aina ya
machonge (incisors), kutokwa majimaji
puani, na maambukizi katika mfumo wa juu wa upumuaji.
Dalili nyingine ni:
* Uchovu na kukosa
nguvu
* Taharuki
* Kuvimba au kushuka
kwa kigubiko cha jicho
* Kusaga meno
* Kunywa sana maji
* Kudondosha hovyo
chakula wakati wa kutafuna
* Muonekano usio
pacha, hususan sungura kuwa na tungamo pamoja na usaha wa mizizi ya meno
* Mabadiliko ya tabia
katika unywaji na ulaji (kama, kupendelea vyakula laini)
* Kukaa kwa kubinuka
na kutopenda kusogea.
Uchunguzi
Daktari wa mifugo anaweza kufanya uchunguzi kwa sungura
kujua tatizo ni nini. Uchunguzi wa njia ya X-Ray kwenye kichwa unaweza
kufanyika pamoja na kupiga X-Ray kwenye kifua ili kuona matatizo katika njia ya
upumuaji.
Uchunguzi katika njia ya mzunguko wa macho (orbital ultrasonography) unaweza pia
kufanyika ili kutoa taswira halisi ya uvimbe ulivyo, na kipimo cha Computed
Tomography (CT scan) kinaweza kutumia kutazama eneo zima la kuzunguka
macho.
Uchunguzi wa mdomo na pua unafanyika pia kwa kutumia sampuli
ya majimaji inayoweza kuchukuliwa kwa sindano kutoka kwenye njia ya mzunguko wa
macho.
Kama kutakuwa na tungamo kwenye njia ya mzunguko wa macho,
kipimo cha biopsy kinaweza kutumika ili kuona kama kuna kansa.
Tiba
Tiba itagemea na sababu za tatizo husika na matokeo ya
uchunguzi wa mwisho. Kama kutakuwa na utando wa ziada wa mafuta nyuma ya macho,
kwa mfano, kupunguza uzito ni jambo linaloshauriwa.
Lakini sungura atapatiwa dawa za antibiotics kuondoa maambukizi ya bacteria.
Kama maambukizi yamesababisha kuwepo kwa usaha, basi
upasuaji utahitaji ambao baadaye utahitaji dawa za kupunguza maumivu pamoja na
jeli maalum za kupaka katika eneo la kuzunguka jicho.
Matunzo
Katika kipindi chhote cha matibabu sungura wako aendelee
kula vizuri, tena vyakula laini ambavyo ataweza kutafuna mpaka atakapokuwa na
uwezo wa kutafuna vyakula vigumu.
Utaendelea kumpa sungura wako vyakula maalum vya punje na
kumhamasisha kula.
Imeandaliwa na www.maendeleovijijini.blogspot.com.
Tupigie: +255 656 331974
Comments
Post a Comment