Featured Post

WANASAYANSI CHIPUKIZI 200 KUANZA KUONYESHA KAZI ZAO KUANZIA LEO AGOSTI 8 HADI 9 JIJINI DAR ES SALAAM

Diana Sosoka (kushoto) na Nadhra Mresa wakiwa a hati zao za ufadhili kutoka taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation. Wanafunzi hao kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana Mtwara, waliibuka washindi wa jumla katika maonyesho ya Sayansi kwa Shule za Sekondari mwaka 2016 yanayoandaliwa na taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST).

Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini Blog
JUMLA ya wanasayansi chipukizi 200 na walimu wao 100 kutoka shule 100 za sekondari Tanzania leo Agosti 8, 2017 wanaanza kuonyesha kazi zao za ubunifu wa sayansi na teknolojia katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

MaendeleoVijijini inafahamu kwamba haya ni maonyesho ya sita ya sayansi na teknolojia kwa wanasayansi hao chipukizi ambayo yameandaliwa na Shirika la Wanasayansi Chipukizi Tanzania (Young Scientists Tanzania – YST) na yatafikia kilele chake kesho Jumatano, Agosti 9, 2017.
Mkurugenzi Mtendaji wa YST, Dkt. Gosbert Kamugisha, ameieleza MaendeleoVijijini kwamba, wanafunzi hao wanatoka katika mikoa takriban 27 ya Tanzania.
“Kwa siku mbili wanasayansi hawa chipukizi wataonyesha kazi zao katika nyanja mbalimbali za sayansi kama vile kemia, fizikia, hesabu, baiolojia, ikolojia, Sayansi ya Jamii na Teknonojia. Kazi nyigi zitakazoonyeshwa zimejikita katika kutoa njia za kukabiliana na matatizo ya afya, kilimo na usalama wa matatizo ya kijamii,” amesema Dkt. Kamugisha.
Maonyesho hayo ambayo ambayo yamedhaminiwa na kampuni ya BG Tanzania ambayo ni mdhamini mkuu, yatashuhudia washindi katika Nyanja mbalimbali wakizawadiwa fedha taslimu, vikombe, medali, vifaa vya maabara pamoja na udhamini wa masomo ya elimu ya juu (scholarships) katika sayansi katika vyuo vikuu mbalimbali.
MaendeleoVijijini inafahamu kwamba, kumekuwepo na ongezeko kubwa la ushiriki wa shule za sekondari kutoka shule 4 mwaka 2011 hadi 100, hatua ambayo imeelezwa imetokana na hamasa ya kupenda kuendeleza masomo ya sayansi kwa shule mbalimbali za sekondari nchini.
Aidha, Programu ya YST ilitokana na jitihada za nchi ya Ireland ambayo ilitumia mfumo wa maendeleo ya elimu kupitia Kundi la Kupambana na Maradhi yanayotokana na Umaskini (CDPC - Combat Diseases of Poverty Consortium) na tangu kuanza kwa maonyesho hayo mwaka 2011, Ubalozi wa Ireland nchini umekuwa miongoni mwa wadhamini.
Kwa miaka zaidi ya 50, MaendeleoVijijini inafahamu kwamba, Ireland imekuwa ikiendesha maonyesho ya sayansi ambayo kimsingi ndiyo yaliyochochea kuanzishwa kwa YST nchini Tanzania na washindi wa jumla wa maonyesho ya YST hupata nafasi ya kuhudhuria maonyesho ya BT Young Scientists jijini Dublin.
Wote kwa pamoja walikuwa wanachukua mchepuo wa Kemia, Balojia na Jiographia (CBG).
MaendeleoVijijini ambayo imekuwa ikiripoti maonyesho hayo kwa mwaka wa nne sasa, ilishuhudia wanafunzi hao wakiangua machozi mara walipotangazwa washindi kufuatia wazo la utafiti wao la ‘Umaskini Siyo Suala la Msingi kwa Wanawake Mkoani Mtwara’ (Poverty Is No Longer An Issue For Women In Mtwara Region) ambapo walizawadiwa nishani, tuzo kubwa na hundi ya Shs. 1.8 milioni.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa wanafunzi walioshiriki maonyesho hayo.
Washindi wa pili walikuwa Bennedict Msangi na William Kiluma kutoka Shule ya Sekondari Mzumbe ambao walikuja na wazo la ‘Umwagiliaji kwa Kutumia Mianzi Mzumbe’ (Bamboo Irrigation System in Mzumbe).
Washindi hao walipata nishani, tuzo na hundi ya Shs. 1.2 milioni.
Zawadi katika maonyesho hayo ziko katika makundi manne ambayo ni Sayansi ya Baolojia na Ikolojia (Biological and Ecological Sciences) iliyodhaminiwa na Kampuni ya uchimbaji gesi ya Statoil kutoka Norway; Sayansi ya Kemia, Hisabati na Fizikia (Chemical, Mathematical and Physical Sciences) iliyodhaminiwa na Kampuni ya Tanga Cement PLC; Sayansi ya Kijamii na Kitabia (Social and Behavioural Sciences) iliyodhaminiwa na Shirika la Concern Worldwide; na Teknolojia (Technology) iliyodhaminiwa na Karimjee Jivanjee Foundation.
Aidha, wadhamini wengine wa maonyesho hayo ni Songas, Taasisi ya Fizikia (Institute of Physics), Read International, Solaris, Karimjee Jivanjee, First Car Rental, Vernier Software & Technology, Tyndall, NCCA, Human Development Innovation Fund (HDIF), SMK, Delfina, Dar es Salaam Serena Hotel, MMI Tanzania, Dar es Salaam Gymkhana Club, Coastal Aviation na DTP.

Orodha ya washindi wa tuzo maalum mwaka 2016 ambao pamoja na nidhani na tuzo, walipata vitita vya Shs. 450,000 kwa kila wazo lililoshinda ni:
Tuzo ya Kupenda Sayansi ya Songas: Moses Minja na Baye Manga Loyola High School jijini Dar es Salaam na utafiti wao ‘Automatic Attendance Taker’.
Tuzo ya Read International: Munira Abdallah na Imran Yusuf kutoka Mucechu Sekondari, Tanga na andiko lao la ‘Local Solution to Bleeding During Injuries’.
Tuzo ya Solaris: Hielonimo John na Vinord Matendo kutoka Kibaha Sekondari, Pwani na utafiti wao wa ‘Kubadili Sauti Kuwa Katika Nguvu ya Umeme’ (Conversion of Sound To Electrical Energy).
Tuzo ya Tyndall: Suleiman Sadik Khamis na Rahma Seleman Jumanne kutoka Mpendae Sekondari, Unguja na andiko lao la ‘The Harmonize Solar Oven’.
Tuzo ya First Car Rental: Julietha Johansen na Edina Alistides kutoka Shule ya Sekondari Bulyakashaju, Kagera na andiko lao la ‘Je, Utapiamlo ni Tatizo la Kiuchumi au Ujinga?’ (Is Malnutrition An Economic Or Ignorance Problem?).
Tuzo ya Vernier: Angelus Albinus na Adolph Tabaro kutoka St. Joseph Kolping, Kagera ambao walikuja na utafiti wao wa ‘The Use of a Spin-Electric Power Drone In Spying, Researching and Providing Optimal Security’.
Tuzo ya HDIF: James James na Michael Nandi kutoka Mbeya Sekondari na andiko lao la Electric Wheel Chair For Disabled. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa tuzo hiyo kwenda Mbeya Sekondari ambao mwaka 2015 Tunu Ngajilo na Ally Salum waliitwaa kutokana na utafiti wao wa Automatic Irrigation System.
Tuzo ya NCCA: Eliah Uledi na Andrew Magoma kutoka Masanga Sekondari, Kigoma na andiko lao la ‘The Survivorship Of Street Children In Kigoma Municipality’.
Tuzo ya Taasisi ya Fizikia (IoP): Gwakisa Gwakabale na Hapiness Katani kutoka Misunkumilo, Katavi na andiko lao la ‘To Investigate The Relationship Between The Expansion of Bimetallic Strip and The Bell Ring by Electric Current’.

Washindi wa makundi mbalimbali:
Sayansi ya Baolojia na Ikolojia:
1. Esther Paschal na Agape Mwalimu kutoka Ndwika Sekondari, Mtwara na utafiti wao wa ‘The Use Of Sweet Basil Plant To Prevent Mosquitoes’.
2. Jackson Nyiga na Victor Magita kutoka Ilboru Sekondari, Arusha na utafiti wao wa ‘Management Of Organic Food Waste’.
3. Doreen Ikula na Rose Rwegasira kutoka Kilakala, Morogoro na utafiti wao wa‘Cholera In Morogoro Municipality’.

Sayansi ya Kemia, Hisabati na Fizikia:
1. Blandina Edmund na Johari Abubakar kutoka Chamaguha Sekondari, Shinyanga ambao utafiti wao ulihusu ‘Emulsifier Fro Increasing Life Span Of Milk’.
2. Claudia Laurent na Sheila Seif kutoka Dk. Salmin Amour Sekondari, Singida na utafiti wao wa ‘Does Fruits Lose Or Gain Vitamin C After Being Picked?’
3. Mathias Kapenda na Jimmy Kibaja kutoka Chidya Sekondari, Mtwara na wazo lao la ‘Kwa Nini Tetemeko la Ardhi Linatokea Katika Mabara Mengine na Siyo Bara la Afrika’ (Why Earthquakes Occur Mostly In Other Continents Than African Continent?).

Sayansi ya Kijamii na Kitabia:
1. Anna Apopolynary Ngairo na Getrude Deogratius Makoye kutoka Debrabant, Dar es Salaam na utafiti wao wa ‘The Use Of Local Resources In Teaching To Make Primary School Pupils Like and Apply Science’.
2. Shabani Mtoi na Munira Juma kutoka Morogoro Sekondari na andiko lao la‘Can Discipline Be Managed In Order To Improve Academic Performance In Secondary Schools?’
3. Annastazia Michael na Dotnatha Ntunga kutoka Ifakara Sekondari na utafiti wao wa ‘Assessing The Effects Of Drug Abuse To Human Being and How To Reduce It’.

Teknolojia:
1. Rashida Remtula Kassu na Luteiya Ahmed Zubeir kutoka Kiembesamaki, Unguja na utafiti wao wa ‘Ultrasonic Frequency Against Flies’.
2. Joshua Mussa na Lucy Konyaki kutoka Binza Sekondari, Simiyu na utafiti wao wa ‘Mashine Rahisi ya Kutotolesha Vifaranga Katika Nchi za Dunia ya Tatu’ (Simple Egg Incubator For Third World Countries). Wanafunzi hao pia walipata Tuzo ya Udhamini (scholarship) wa shahada ya kwanza kutoka taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation.
3. Nancy Godfrey na Grace Temu kutoka Edmund Rice Sinon, Arusha na utafiti wao ‘A Low Cost Vegetable Cutting Machine’.


Comments