- Get link
- Other Apps
Featured Post
RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AMUAPISHA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAWI PIA APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO WA MABALOZI WATANO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Posted by
Unknown
on
- Get link
- Other Apps
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akimuapisha Benedict Mashiba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Balozi wa Tanzania nchini Malawi Benedict Mashiba akila kiapo cha
uadilifu kwa Viongozi mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Balozi wa
Tanzania nchini Malawi Benedict Mashiba mara baada ya tukio la uapisho Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akipokea Hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni
Kim Doahn, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn akipigiwa wimbo wa
Taifa mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za
Utambulisho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana
na Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn mara baada ya kumaliza
mazungumzo pamoja na kupokea Hati za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn katikati akipigiwa
wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za
Utambulisho.
Balozi wa Indonesia hapa nchini Prof. Ratlan Pardede(katikati ) akipigiwa
wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za
Utambulisho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Indonesia hapa nchini Prof.
Ratlan Pardede, Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Indonesia hapa nchini Prof. Ratlan
Pardede, Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Vatican hapa nchini Mwadhama
Askofu Mkuu Marek Solcynski, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akimshukuru Balozi wa Vatican hapa nchini Mwadhama Askofu Mkuu Marek Solcynski
mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini.
Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef Wachter akipigiwa wimbo wa Taifa mara baada
ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kukabidhi Hati zake Utambulisho.
Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef Wachter akijitambulisha kabla ya kuwasilisha
Hati zake za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef Wachter mara baada ya kupokea hati zake za
Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akipokea Hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Richard
Tumisiime Kabonero Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akipiga ngoma ya Brass Bendi ya Jeshi la Polisi ambayo ilifika Ikulu kwa ajili
ya mapokezi ya Mabalozi mbalimbali kutoka nje ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika picha ya pamoja na Brass Bendi ya Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar
es Salaam. PICHA NA IKULU
Comments
Post a Comment