- Get link
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- Other Apps
Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akizungumza na wafanyabiashara wanaotoa
huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA),
wakati alipofanya kikao cha pamoja, leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Kaimu MKurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi (Kulia), wakati
alipokagua sehemu ya kuingilia abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyabiashara
wanaotoa huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
(JNIA) wakimsikiliza Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame
Mbarawa (Hayupo pichani) wakati alipofanya kikao cha pamoja, leo Jijini Dar es
Salaam.
Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wafanyabiashara wanaotoa
huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA),
wakati alipofanya kikao cha pamoja, leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa Mwezi mmoja kwa wafanyabiashara wanaotoa
huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA)
kulipa kodi ya Majengo kama mikataba yao inavyolekeza.
Waziri Mbarawa ametoa agizo
hilo leo wakati alipokutana na wafanyabiashara hao ili kujadili changamoto
mbalimbali zilizopo na jinsi ya kuzitatua ili kuendelea kutoa huduma bora
katika uwanja huo.
“Kulipa kodi za majengo hapa ni
suala la lazima, hivyo ifikapo Septemba mwishoni nataka kuona wafanyabiaashara
wote mmeshalipa kodi ya pango, makusanyo haya ni muhimu kwetu ili tuendelee na
hatua nyingine za uboreshaji wa viwanja vya ndege na huduma nyinginezo.” Amesisitiza
Profesa Mbarawa.
Aidha, Profesa Mbarawa ameutaka
uongozi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA), Kuhakikisha mikataba
yote ya upangishaji wa majengo inapitiwa upya na kufanyiwa marekebisho ili
thamani ya fedha iendane na wakati huu.
Profesa Mbarawa amewahimiza
wafanyabiashara hao kubadilika na kuendana na mabadiliko ya Sayansi na
Teknolojia ili kuweza akuendana na ushindani wa kibiashara uliopo ndani na nje
ya nchi.
Ameongeza kuwa Serikali
itaendelea kujenga mazingira mazuri kwa wafanyabiashara nchini ili waweze
kufanya biashara zao ili kujiingizia kipato binafsi na kukuza pato la Taifa.
Katika hatua nyingine Profesa
Mbarawa amekagua sehemu ya kuingilia abiria katika uwanja huo ambapo amesema
Serikali itaweka mpango maalum wa muda mfupi kwa wasafiri wanaoenda nje
kutotumia muda mrefu katika ujazaji wa fomu wakiwa uwanjani hapo.
“Kwa kushirikiana na taasisi
zote zinazotoa huduma katika uwanja huu tutaweka mpango maalum utakaowezesha wasafiri
kuhudumiwa kwa haraka na kwa muda mfupi, Msafiri yoyote anataka huduma za
haraka ili waweze kuwahi na sisi tutahakikisho tunakidhi mahitaji ya wateja,”
amesisitiza Profesa Mbarawa.
Kwa upande Kaimu MKurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi amesema
Mamlaka imeshapitia mikataba yote ya wafanyabiashara kiwanjani hapo na hatua
inayofata ni kufatilia madeni yote ili kuboresha huduma katika kiwanja hicho.
Bw. Msangi ameongeza kuwa kwa
yale madeni ambayo hayataweza kulipwa kwa wakati taratibu za kisheria
zitafuatwa.
Comments
Post a Comment