Featured Post

MHANDISI LWENGE AIPONGEZA WIZARA YA KILIMO MIFUGO NA UVUVI KWA ELIMU WANAYOITOA KUHUSU UTUNZAJI WA MALISHO

Mgeni rasmi Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge Akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Mgeni rasmi Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge akisalimiana na Afisa habari wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Ndg Issa Sabuni mara baada ya kutembelea Maonesho ya wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Mgeni rasmi Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Maonesho ya wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Mgeni rasmi Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge akipata ufafanuzi kuhusuidara ya uzalishaji wa mifugo na masoko inavyofanya kazi mara baada ya kutembelea Maonesho ya wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Mgeni rasmi Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge akipata ufafanuzi kuhusuchangamoto za masoko ya bidhaa zinazotengenezwa kwa ngozi kutoka kwa meneja wa Robi Leather Product Bi Rose Otieno mara baada ya kutembelea Maonesho ya wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Mgeni rasmi Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge alipowasili kwenye Maonesho ya wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
 
Na Mathias Canal, Lindi

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Greyson Lwenge ameipongeza Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kwa elimu wanayoitoa kwa wananchi kuhusu utunzaji wa malisho ambayo ni nyasi na mikunde kwa ajili ya mifugo kwani jambo hilo litawawezesha wananchi kuwa na mifugo yenye afya bora.

Mhandisi Lwenge ameyasema hayo alipotembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi idara ya uzalishaji wa mifugo na masoko wakati wa Maonesho ya wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Alisema kuwa malisho ni chakula cha msingi cha mifugo ambacho kinajumuisha aina mbalimbali za nyasi na mikunde.

Pamoja na kutolewa elimu juu ya umuhimu wa utunzaji wa malisho lakini pia amesisiza zaidi wizara ya kilimo kutoa elimu kuhusu utunzaji wa malisho hayo jambo ambalo litawawezesha wafugaji kuipatia mifugo yao chakula bora na cha kutosha wakati wote.

Zipo faida nyingi za kupanda malisho ikiwa ni pamoja na kurahisisha upatikanaji wa chakula cha mifugo chenye viini lishe kama wanga, protini madini na vitamin.

Faida Zingine ni kurutubisha ardhi hasa malisho aina ya mikunde sambamba na kuzuia mmomonyoko wa ardhi.

Mhandisi Lwenge amesema kuwa malisho ndio chakula kikuu cha mifugo inayochengua (Ng’ombe, mbuzi, kondoo, punda na ngamia.

MWISHO

Comments