MGEJA AMSHUKI KINANA, ATAKA AACHE KUWAHADAA NA KUWAFANYA WATANZANIA WATOTO

Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana

Na Hastin Liumba,KigomaMWENYEKITI wa Tanzania Mzalendo foundation (Taasisi inayoshughulikia utawala bora na haki za binadamu)  Khamis Mgeja amemtaka katibu mkuu wa CCM Taifa Abdulrahaman Kinana aache kuwahadaa na kuwafanya Watanzania kuwa watoto kwa kukiri hadharani madudu yaliyofanywa na serikali za awamu zilizopita kuwa yanarekebishwa na serikali ya awamu ya tano.

Mgeja alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari mkoani Kigoma akiwa njiani kuelekea Dar-es-Salaam.
Alisema Kinana alisema maneno hayo hivi majuzi katika ziara ya Rais Dk John Magufuli mkoani Tanga alipopewa nafasi ya kuzungumza na wananchi eneo la Mkanyageni wilaya ya Muheza.
Aidha Mgeja alisema na kuanza kumnukuu Kinana kuwa …’Jitihada zinzofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kurekebisha makosa ni sahihi na hakuna tatizo lolote kufanya hivi kutokana na ukweli kuwa awamu ya seriakali zote zilizopita na ya sasa ni za CCM na kama kuna makosa yaliyofanywa na awamu zilizopita hakuna shida kwa sababu hata anayerekebisha ni wa CCM lakini kama alieharibu ni wa CCM mimi sioni tatizo hivyo tuache kualalamika’,mwisho wa kumnukuu.
Mgeja alisema na kuongeza amesikitishwa na kauli ya Kinana ambaye ni kaka yake anayemheshimu sana lakini kauli hizo zimemsikitisha yeye na watanzania, ni nyepesi mno hasa katika maswala mazito ambayo taifa limeathirika na uongozi mbovu wa serikalizilizopita ikiwemo ufisadi,wizi,uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya madaraka.
"Kinana atambue kuwa leo hii taifa linanuka umasikini wa kutupwa kwa sababu ya mikataba mibovu ya rasilimali za nchi zilizofanywa  kwa makusudi na watawala waliokabidhiwa dhamana na wananchi ikiwemo na CCM na kupelekea wananchi kushindwa kunufaika na rasilimali zao walizotunukiwa na Mungu," alisema.
Alisema wote tulitegemea Kinana atoe tamko kama chama aelekeze serikali ya awamu ya tano na watawala wote walioitumbukiza nchi katika lindi la umasikini wafikishwe mahakamani haraka iwezekanavyo akiwemo rais mstaafu Benjamin Mkapa kama wanavyofanya nchini Malawi kwa rais mstaafu Joyce Banda kwa ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.
‘Kauli alizotoa Kinana sijui anamfurahisha nani kwani makosa hayo yaliyofanywa na serikiali zilizopita siyo ya kurekebishwa kwa hiyo hayarekebishiki zinahitaji hatua kali za kisheria watanzania wanataka waone kuliko kulindana kama kuna kinga ziondolewe kwa misingi ya katiba na sheria.’aliongeza.
Mgeja alitegemea Kinana kama katibu mkuu wa CCM taifa awaombe radhi watanzania kwa yale yaliyofanywa ya ufisadi,wizi na matumizi mabaya ya madaraka kwa serikali zilizopita kama chama chake cha CCM ndicho kilichopewa dhamana kuongoza taifa hili hivyo ubadhirifu huo kama chama lazima kibebe lawama na kuwajikiba kwa wananchi.
Alisema na kudai Kinana atambue kuwa watazania wa leo siyo wa kudanganyika kwani wanajitambua hivyo hakuna wa kuwadanganya wala wa kuwahadaa