- Get link
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- Other Apps
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni, akizungumza na watumishi wa Kitengo cha Jeshi la Polisi cha Kuzuia Dawa
za Kulevya pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati alipofanya
ziara katika kitengo hicho kilichopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam,
ambapo aliwaagiza kuhakikisha wanapambana na uingizwaji wa dawa hizo kupitia
bandari bubu na mianya yote ya uingizwaji na usambazaji. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Kamishna wa Kitengo cha Jeshi la Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, DCP Mkonyi,
akitoa taarifa fupi ya hali ya uzuiaji wa Dawa za Kulevya mbele ya Naibu Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, alipofanya ziara katika kitengo hicho
kilichopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, ambapo
aliwaagiza kuhakikisha wanapambana na uingizaji wa dawa hizo kupitia bandari
bubu na mianya yote ya uingizwaji na usambazaji. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisomewa
takwimu za matukio ya ukamataji wa Dawa za Kulevya na mmoja wa afisa wa Kitengo cha Jeshi la Polisi cha Kuzuia Dawa
za Kulevya wakati alipofanya ziara
katika kitengo hicho kilichopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, ambapo
aliwaagiza kuhakikisha wanapambana na uingizwaji wa dawa hizo kupitia bandari
bubu na mianya yote ya uingzwaji na usambazaji. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiongozana
na Naibu Kamishna wa Polisi, DCP Mkonyi, wakati alipotembelea Kitengo cha Jeshi la Polisi cha Kuzuia Dawa za
Kulevya kilichopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, ambapo aliwaagiza
kuhakikisha wanapambana na uingizwaji wa dawa hizo kupitia bandari bubu na
mianya yote ya uingzwaji na usambazaji. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Comments
Post a Comment