- Get link
- Other Apps
Featured Post
MASAUNI AKAGUA UJENZI WA VITUO VYA POLISI, AFANYA MKUTANO NA ASKARI WA USALAMA BARABARANI NA MADEREVA BODABODA
Posted by
Unknown
on
- Get link
- Other Apps
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
akimuuliza maswali Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, wakati
alipotembelea Ujenzi wa Kituo cha Polisi Mjimwema, Wilayani Kigamboni kukagua maendeleo ya ujenzi huo. Kulia ni
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Gilles Muroto na anayefuatia ni Mkuu
wa Utawala Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Benadict Kitalika .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
Mkuu
wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, akimuonyesha eneo linapotakiwa kujengwa
kituo cha Polisi Kibada, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya naibu waziri,wilayani
Kigamboni, Dar es Salaam. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(kulia), akikagua moja ya chumba cha mahabusu ndani ya kituo cha Polisi
Mwasonga, wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya polisi wilayani Kigamboni,
jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Hashim Mgandilwa. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Muonekano
wa nje wa Kituo cha Polisi cha Mwasonga kilichopo wilayani Kisarawe, kikiwa katika hatua za mwisho kabla ya ujenzi wake
kukamilika. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza
na madereva bodaboda wakati wa ziara ya kikazi wilayani Kigamboni ambapo
aliwaasa madereva hao kufuata sheria za usalama barabarani pindi wafanyapo
shughuli zao ili kuepuka ajali. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Muendesha
Bodaboda wa Wilaya ya Kigamboni, Said Athumani, akimuuliza maswali Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo
pichani), wakati wa Mkutano ulioitishwa na naibu waziri huyo wakati wa ziara ya
kikazi wilayani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Muendesha
Bodaboda wa Wilaya ya Kigamboni, Fredrick Swai, akimuuliza swali Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo
pichani), wakati wa Mkutano ulioitishwa na naibu waziri huyo wakati wa ziara ya
kikazi wilayani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Comments
Post a Comment