MAKAMU WA RAIS AWASILI LINDI KUHUDHURIA KILELE CHA NANE NANE

 Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge wa Mtama, Mhe. Nape Nnauye.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea taarifa ya mkoa wa Lindi inayosomwa naMkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi mara baada ya kuwasili mkoani Lindi tayari kwa kuhudhuria kilele cha sherehe za wakulima (Nane Nane). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Lindi na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi.
Makamu wa Rais amewasili mkoani Lindi tayari kwa kuhudhuria kilele cha sherehe za  siku ya Wakulima (Nane Nane) ambapo kitaifa zinaadhimishwa mkoani Lindi.
Katika Uwanja wa ndege wa kikwetu Lindi, Makamu wa Rais pia alipokelewa na Viongozi wa Chama na Serikali pamoja na Vikundi vya ngoma ambavyo vilimlaki kwa nyimbo mbali mbali.
Kesho siku ya Kilele cha sikukuu ya Wakulima (Nane Nane), Makamu wa Rais  atapata fursa ya kutembelea mabanda yakiwemo ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi katika maonesho hayo kwenye viwanja vya Ngongo kisha kuhitimisha kwa kuhutubia Wananchi  kwenye maonesho hayo.