- Get link
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- Other Apps
Mhandisi
Mshauri wa barabara ya Mayamaya – Mela (km 99.35), Eng. Leornado Licari, akitoa
maelezo ya mradi wa barabara hiyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (wapili kushoto),
alipofanya ukaguzi mkoani Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng.
Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa mkandarasi wa kampuni ya CHICO
anayejenga sehemu ya barabara ya Mayamaya – Mela (km 99.35), alipofanya ukaguzi
mkoani Dodoma.
Muonekano
wa sehemu ya juu ya daraja la Kelema lenye urefu wa mita 205 linalounganisha
wilaya ya Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng.
Joseph Nyamhanga, akikagua kingo za daraja la Kelema lenye urefu wa mita 205
linalounganisha wilaya ya Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng.
Joseph Nyamhanga (wapili kushoto), akiwa na wataalamu wanaosimamia ujenzi wa
barabara ya Mayamaya – Mela (km 99.35), inayojengwa kwa kiwango cha lami mara
baada ya kuikagua mkoani Dodoma. Wanne kushoto ni Mkurugenzi wa barabara Eng.
Ven Ndyamukama.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng.
Joseph Nyamhanga, akikagua sehemu ya barabara ya Mela – Bonga (km 88.8),
inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Manyara.
Ujenzi
wa barabara ya Dodoma – Babati kwa kiwango cha lami sehemu ya Mela – Bonga (km
88.8), ukiendelea.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng.
Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS),
mkoa wa Manyara, Eng. Bashiri Rwesingisa (kulia), na mkandarasi wa Kampuni ya
China Railway Seventh Group Co. Ltd anayejenga sehemu ya Mela – Bonga (km
88.8), mkoani Dodoma.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga,
amewaagiza Mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma na Manyara
kuhakikisha wanatafuta eneo la kujenga kituo cha mizani ili kudhibiti madereva
wanaozidisha uzito katika barabara ya Dodoma- Babati (km 263), inayojengwa kwa
kiwango cha lami.
Akizungumza katika eneo la
Bonga, mkoani Manyara Eng. Nyamhanga, amesema kuwa barabara hiyo ambayo
inatarajiwa kukamilika baadae mwezi huu inahitaji uwepo wa mizani kwa haraka
ili kudhibiti magari yanayozidisha uzito
na kuharibu barabara.
"Hakikisheni mnatafuta eneo la kujenga mizani ndani ya miezi miwilli ambapo wakandarasi bado wapo hapa ili iwe rahisi kwenu kumtumia mmoja wa wakandarasi hawa kuweza kujenga kituo hiki haraka, uwepo wa mizani hii utasaidia kudhibiti magari makubwa yanayozidisha uzito", amesema Katibu Mkuu Nyamhanga.

Aidha, Eng. Nyamhanga
amewaagiza mameneja wote nchini kuchukua hatua kali za kisheria kwa watu wote
wanaopitisha mifugo katika barabara ili kudhibiti uharibifu wa barabara.
Amewataka madereva wote nchini kuendesha magari yao kwa tahadhari na kuzingatia alama za barabarani ili kudhibiti ajali zinazoepukika.
Amewataka madereva wote nchini kuendesha magari yao kwa tahadhari na kuzingatia alama za barabarani ili kudhibiti ajali zinazoepukika.
Katibu Mkuu Nyamhanga ametoa wito
kwa wananchi wanaoishi kando ya barabara hiyo kuhakikisha wanatumia fursa ya
kukamilika kwa barabara hiyo kwa ajili ya kuleta maendeleo katika maeneo yao
ili kukuza uchumi kwa familia zao na Taifa kwa ujumla.
Amemataka mkandarasi wa
sehemu ya barabara ya Mela - Bonga (km88.8) kuhakikisha anakamilisha kazi
zilizobaki kwa wakati na kwa viwango vilivyo kwenye mkataba.
Katika hatua nyingine, Eng.Nyamhanga, ametembelea na kukagua barabara ya Mayamaya- Mela (km 99.35) kwa kiwango cha lami na daraja la Kelema lenye urefu wa mita 205 na kuridhishwa na ujenzi wake na kumtaka mkandarasi wa mradi huo kukabidhi mradi huo ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.

Kwa upande wake, Mhandisi
Mshauri wa barabara ya Mayamaya- Mela (km 99.35), Leornado Licari,
amemhakikishia Katibu Mkuu huyo kumaliza mradi huo kwa wakati kwani kazi
zilizobaki kwa sasa ni ndogo kama kumaliza tabaka la mwisho la lami na uwekaji
wa alama za barabarani.
Barabara ya Dodoma- Babati (km
263) ni sehemu ya barabara kuu ya kaskazini (Great North road), inayoanzia
Capetown nchini Afrika Kusini hadi Cairo nchini Misri ambapo hapa nchini
barabara hiyo inayopitia Tunduma mkoani Mbeya, hadi Namanga mkoani Arusha ina
urefu wa kilomita 1500,hivyo kukamilika kwa sehemu ya barabara ya Dodoma –
Babati (km 263), kunaiunganisha barabara yote kutoka Capetown hadi Cairo
yenye urefu wa kilomita 100000 kwa
kiwango cha lami.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Comments
Post a Comment