Featured Post

DKT TIZEBA ATEUA WAJUMBE WA BODI ZA WAKURUGENZI WA BODI ZA MAZAO CHINI YA WIZARA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI



Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew J. Mtigumwe anawaarifu kuwa Mheshimiwa Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Dkt. Charles J. Tizeba (Mb), kwa mamlaka aliyopewa chini ya sheria mbalimbali za Mazao amefanya uteuzi wa wajumbe wa Bodi za Wakurugenzi za Bodi za Mazao kama ifuatavyo:


A: Bodi ya Kahawa Tanzania:

Kwa mujibu wa kifungu cha 1(1)-(4) cha Sheria ya Kahawa ya Mwaka 2001 kama ilivyorekebishwa na Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Mazao Na.20/2009 Mhe. Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Kahawa Tanzania:  

1.                               Bibi Fatima Aziz Faraji
2.                               Bw. Twahir S. Nzallawahe
3.                               Bw. Titus Thobias Stanslaus Itigereize
4.                               Prof. Faustine Karrani Bee
5.                               Bw. Boaz A. Mwalusamba
6.                               Bibi  Elizabeth Siwa Bwire
7.                               Bw. Robert Seleman Mayongela
8.                               Bw. Daudi Felician Magayane
9.                               Bw. Amiri Hamza

B: Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

Kwa  mujibu wa  kifungu cha 1(1)  cha Sheria  ya Shirika la  Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika  ya  Mwaka 1982 kama ilivyofanyiwa Marekebisho  na Sheria  Na.9  ya mwaka 2005, 2009 Mhe. Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika Tanzania:

1.           Dkt. Tito B. Haule
2.           Bibi Mary Maganga
3.           Prof. Faustine Karrani Bee
4.           Bw. Aziz J. Dachi
5.           Bibi Mechtilda Yahaya Zimbwe

C: Bodi ya Mkonge Tanzania

Kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 1(i) cha Jedwali katika Sheria ya Mkonge ya mwaka 1996 kama ilivyorekebishwa na Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Mazao Na.20/2009, Mhe. Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Mkonge Tanzania:

1.           Eng. Mark W. Njiu
2.           Bw. Abdallah Ngereza
3.           Bw. Deogratias Ruhinda
4.           Bw. Freddie Robert Semwaiko
5.           Bibi Laddy Aminiel Swai
6.           Bw. Revelian Ngaiza
7.           Bibi Nyambilila Amuri
8.           Bi. Betty Eliezer Machangu

D: Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko

Kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Na.19 ya Mwaka 2009, Mhe. Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania:

1.           Bw. Celestine Bugami Bulima
2.           Bw. Sylivanus M. Chacha
3.           Bibi Getrude J Haule
4.           Bw. David Issaya Dyoya
5.           Bw. Shabila Patrick Mussa
6.           Bw. Enock Seif Ananidze
7.           Bw. Deogratias Bugomola Kumalija
8.           Bibi Zakia Stephano Lwamala
9.           Bw. Ali Gugu
10.       Bw. Mukara M. Mugini
11.       Bw. Fredricks Simon Towo
12.       Bibi Monica Ngezi Mbega

E: Tume ya Maendeleo ya Ushirika

Kwa mamlaka aliyopewa Chini ya  Kifungu cha  7(1) Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya Mwaka 2013, Mhe. Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi  amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika.

1.   Bw. Lucas Dudumila Mataba
2.   Bw. Robert Busumabu
3.   Bw. Mudhihir Mudhihir
4.   Bw. Abdul Jabir Malombwa
5.   Bibi Salome Tondi
6.   Bw. Edward Maura
7.   Bw. Mibavu Gungu Mohamed
8.   Bw. Athuman L. Mahadhi
9.   Bibi Elizabeth C. Makwabe
10.  Dkt. Lucy Ssendi

Uteuzi huo wa wajumbe wa Bodi zote ni wa miaka mitatu (3)  na unaanzia tarehe 10 Agosti, 2017. Wajumbe hao wa Bodi wanapaswa kukutana mapema. Maelekezo husika yatatolewa kupitia Menejimenti za taasisi husika.

Katibu Mkuu na Menejimenti ya Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi inawapongeza wajumbe wote kwa uteuzi huu. Ni matumaini ya Serikali kuwa, wajumbe watashirikiana kwa dhati na Serikali na Wadau kwa ujumla katika kusaidia kuleta  maendeleo ya Sekta ya Kilimo.
<!--[if gte mso 9]>

Comments