- Get link
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- Other Apps
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali
ya Rufaa ya Dodoma Dkt. Samwel Seseja (Wa Pili kushoto), akitoa taarifa ya
namna mfumo wa TEHAMA unavyofanya kazi katika hospitali hiyo kwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria
Sasabo (kushoto), alipokagua matumizi ya TEHAMA katika hospitali hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo (Wa
Pili kulia), akiwasili katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kukagua utendaji wa
mifumo ya TEHAMA katika hospitali hiyo. Wa Kwanza kushoto ni Afisa TEHAMA wa
hospitali hiyo ni Bi. Sylivia Urio.
Muonekano wa mifumo ya TEHAMA
iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma ambayo itawezesha hospitali hiyo
kutoa huduma kwa njia ya kisasa na kwa urahisi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bi. Rachel Chuwa, akifafanua
jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo (kushoto).
Imetolewa na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo, amezungumzia
umuhimu wa taasisi za umma zilizo chini ya mradi wa Benki ya Dunia kuhakikisha
mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), iliyofungwa
inafanyakazi mara moja ili kuongeza tija na ufanisi katika kuhudumia wananchi.
Akizungumza
wakati wa ziara yake ya kukagua ufanisi wa matumizi ya TEHAMA katika hospitali
ya rufaa ya Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Dkt. Sasabo amewataka viongozi wa taasisi hizo kuhakikisha
mifumo hiyo inakamilika na kuanza kazi mara moja.
“Hakikisheni
ifikapo mwezi Septemba mawasiliano yenu na huduma zenu zilizounganishwa kwenye
mifumo ya TEHAMA inafanyakazi ili kurahisisha utendaji na kuiongezea Serikali mapato”,
amesema Dkt. Sasabo.
Dkt.
Sasabo amemtaka Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya rufaa ya Dodoma Dkt. Samweli
Seseja, kuhakikisha hospitali hiyo inakuwa na mfumo maalum wa mawasiliano
utakaowezesha kuboresha huduma katika hospitali hiyo na kumudu ongezeko la watu
katika Manispaa ya Dodoma.
Akiwa
wilayani Bahi, Katibu Mkuu huyo wa mawasiliano
amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi Bi, Rachel Chuwa kuhakikisha
mifumo ya Tehama iliyofungwa katika
ofisi za halmashauri hiyo na katika shule za sekondari wilayani humo inafanyakazi
mara moja ili kuendana na malengo ya serikali katika utoaji wa huduma bora, za
kisasa na kwa wakati kwa wananchi wake na hivyo kuiwezesha Tanzania kufikia
malengo ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Serikali
imekuwa ikihamasisha matumizi ya TEHAMA katika taasisi zake zikiwemo ofisi, shule,
hospitali na vituo vya polisi ili
kuboresha huduma na kuwezesha uwazi katika ukusanyaji wa mapato na hivyo
kuhamasisha wananchi kuchangia huduma kwa hiari.
Imetolewa na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.
Comments
Post a Comment