Featured Post

DKT. MPANGO AITAKA WIZARA NA TAASISI ZAKE KUWAHUDUMIA WANANCHI KIKAMILIFU

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akisalimiana na watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na baadhi ya Taasisi zilizo chini ya Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 24 ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo.
 

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) akipata ufafanuzi wa Utaratibu wa malipo ya kiinua mgongo, pensheni na mirathi alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tume ya Mipango Bi. Joyce Mkinga pamoja na Mkuu wa Hazina Ndogo Lindi Bi. Pili Kamali
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) anayesaini kitabu cha wageni, katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Fedha alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika viwanja vya Nanenane, Ngongo, mkoani Lindi.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara na Taasisi zake walioshiriki Maonesho ya 24 ya Nanenane, yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.  Kulia kwake ni Meneja Takwimu Mkoa wa Lindi Bw. Moses Sagala, kushoto kwake ni Mkuu wa Hazina Ndogo Lindi Bi. Pili Kamali, na Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amewataka watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake kuwahudumia wananchi kwa uadilifu ili kujenga uaminifu kwa wananchi na Serikali yao.

Dkt Mpango aliyasema hayo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika viwanja vya maonesho Nanenane katika eneo la Ngongo mkoani Lindi.

Alisema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango inategemewa na wananchi wengi hivyo ni vyema wahudumiwe vizuripamoja na kutoa elimu kwa umma vya kutosha ili waweze kuelewa na kuridhika na huduma zinazotolewa na wizara.

“Tujitahidi kuwaelezea wananchi juu ya kazi na huduma zetu ili waweze kuzitumia kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla na tuweze kufikia uchumi wa viwanda kama lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ilivyojipangia ” Alisisitiza Dkt. Mpango.

Kauli mbiu ya maonesho ya Nanenane mwaka huu ambayo ni ya 24 kufanyika kitaifa huku yakifanyika mwaka wan ne mfululizo mkoani Lindi inasema “Zalisha kwa tija mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati”.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
Ngongo Lindi

Comments