Featured Post

MASAUNI AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA MAHAKAMA YA UMOJA WA MATAIFA (UNMICT-TAWI LA ARUSHA), JIJINI DAR



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkaribisha Mkuu wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa (UNMICT), Ofisi ya Arusha, Samwel Akorimo wakati viongozi wa Mahakama hiyo walipomtembelea kiongozi huyo wa Wizara, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya UNMICT na Wizara hiyo. Katikati ni Msajili wa Mahakama hiyo, Dk. Elias Olufemi.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na  Mkuu wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa (UNMICT), Ofisi ya Arusha, Samwel Akorimo (wapili kushoto) na Msajili wa Mahakama hiyo, Dk. Elias Olufemi (kushoto), wakati walipomtembelea Wizarani kwa lengo la kujadili  masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya UNMICT na Wizara hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa (UNMICT), Ofisi ya Arusha, Samwel Akorimo (kulia) wakati alipokuwa akifafanua jambo kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya UNMICT na Wizara hiyo. Wapili kulia ni Msajili wa Mahakama hiyo, Dk. Elias Olufemi. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Naibu Waziri, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kulia),  Mkuu wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa (UNMICT), Ofisi ya Arusha, Samwel Akorimo (wapili kulia), Msajili wa Mahakama hiyo, Dk. Elias Olufemi (watatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wengine mara baada ya Mhandisi Masauni kufanya mazungumzo na ujumbe huo, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo.   Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
*****************************************************************************

Comments