AZAMA YATANGULIWA FAINALI KUISUBIRI YANGA AU SIMBA

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
BAO pekee la kiungo Frank Raymond Domayo limetosja kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Taifa Jang’ombe katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Domayo alifunga bao hilo dakika ya 33 kwa shuti la umbali wa mita 19, baada ya kuwazidi mbinu viungo wa Taifa Jang’ombe.
Na kwa ushindi huo, Azam FC inakwenda fainali ambako itakutana na mshindi kati ya Simba na Yanga Ijumaa. Simba na Yanga zitamenyana kuanzia Saa 2:15 usiku wa leo katika Nusu Fainali ya pili Uwanja wa Amaan.
Pamoja na kufungwa, Taifa Jang’ombe walicheza vizuri na kutengeneza nafasi, lakini bahati haikuwa yao jioni ya leo.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe/Himid Mao dk46, Gardiel Michael, Aggrey Morris, Yakubu Mohammed, Stephan Mpondo/Abdallah Kheri dk79, Joseph Mahundi/Enock Atta Agyei dk75, Frank Domayo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor’ na Yahya Mohammed/Shaaban Iddi dk59.
Taifa Jang’ombe; Ahmed Suleiman, Omary Yussuf, Hassan Msabah, Abdallah Shaibu, Samir Yahya, Khatib Simai/Arafat Suleiman dk53, Adam Ibrahim, Ali Mkanga, Yahya Tumbo/ally badru dk53, Meta Apingi/Hassan Salum dk74 na Mohammed Said.
CHANZO: BIN ZUBEIRY BLOG