Featured Post

MALEZI BORA NI MSINGI WA MAFANIKIO KATIKA ELIMU NA TAIFA

Wanafunzi wa shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings wakionesha umahiri wao katika michezo wakati wa siku ya wazazi na mahafali ya wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Diwani wa Kata ya Segerea jijini Dar es salaam Edwin Mwakatobe akitoa hotuba wakati wa siku ya wazazi na mahafali ya wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Shule shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings Bw. Julius Rutabanja akitoa hotuba wakati wa siku ya wazazi na mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings Machange Kisyeri akitoa neno la shukrani mara baada ya Mgeni Rasmi na Diwani wa Kata ya Segerea jijini Dar es salaam Edwin Mwakatobe (hayupo pichani) mara baada ya kutoa hotuba wakati wa siku ya wazazi na mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa elimu ya awali katika hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Aloyce Siame shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings akitoa taarifa ya shule wakati wa siku ya wazazi na mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Wanafunzi wa Elimu ya Awali ambao wamehitimu wakisoma risala kwa  Mgeni Rasmi Diwani wa Kata ya Segerea jijini Dar es salaam Edwin Mwakatobe pamoja na wazazi (hawapo pichani) wakati wa siku ya wazazi na mahafali ya wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings Jackson Nziku akionesha wageni pamoja na wazazi jaribio la namna ya kuchuja maji machafu kwa matumizi ya kawaida wakati wa siku ya wazazi na mahafali ya wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Aliyevaa suti na tai nyekundu ni Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo Machange Kisyeri.
Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings Irene Valentino akionesha wageni pamoja na wazazi jaribio la namna ya uoteshaji wa mbegu na umuhimu wa maji, mwanga na hewa wakati wa siku ya wazazi na mahafali ya wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
 
Baadhi ya wazazi wakifuatilia michezo wakati wa siku ya wazazi na mahafali ya wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Wanafunzi wa elimu ya awali wakati wa siku ya wazazi na mahafali yao katika shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
Mgeni Rasmi na Diwani wa Kata ya Segerea jijini Dar es salaam Edwin Mwakatobe (aliyevaa skafu) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi na walimu wa shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
(Picha na Eleuteri Mangi) 

Na Eleuteri Mangi
Wazazi na walezi wametakiwa kusimamia watoto wao ili kuhakikisha wanapata elimu stahiki wakati wote wanapokuwa shuleni hatua ambayo itawasadia maisha yao na kupata viongozi wazalendo kwa nchi yao.
Kauli hiyo imetolewa na Diwani wa Kata ya Segerea Edwin Mwakatobe mwishoni mwa wiki wakati wa siku ya wazazi na mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings jijini Dar es salaam.
“Tuwasimamie watoto tusiwakatie tamaa, wasiposimamiwa vizuri sasa wakiwa katika umri wa masomo, tutawapoteza na hivyo kuharibu maisha yao ya baadae, hii ni rasilimali kwa familia na kwa taifa” alisema Diwani Mwakatobe.
Katika kuhakikisha shule inatoa elimu yenye tija kwa wanafunzi na wazazi, Diwani Mwakatobe alisema kuwa amefurahishwa na shule ya Genius Kings kuitikia wito wa Serikali kwa wawekezaji binafsi ndani ya nchi kuchangia jitihada za kuendeleza sekta ya elimu nchini.
Ili kuhakikisha mafanikio katika sekta ya elimu yanakuwa endelevu na Watanzania wengi wananufaika na jitihada za wawekezaji binafsi, Diwani Mwakatobe alisema kuwa ni lazima kila mdau wa elimu atimize wajibu wake kikamilifu ikiwemo kuendesha shule kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi zilizowekwa.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi, mmoja wa Wakurugenzi wa Shule hiyo Bw. Julius  Rutabanja alinukuu maneno ya maandiko Matakatifu kutoka Mithali 22:6, yanayosema “Mlee mtoto katika njia impasayo kuienenda, naye hataiacha hadi uzeeni mwake”.
Bw Rutabanja aliongeza kuwa msingi mkubwa wa shule yao sio tu kutoa elimu bora, kuinua kiwango cha elimu nchini na kuibua vipaji vya watoto, bali ni pamoja na kuhakikisha watoto hao wanapata malezi ya kimwili, kiroho na kimaadili. 
Awali akitoa taarifa ya shule kwa Mgeni Rasmi na wageni waalikwa, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Aloyce Siame alisema kuwa tangu kuanzishwa shule hiyo Januari 7, 2008 imekuwa na mafanikio makubwa katika kutoa taaluma bora kwa ongezeko kubwa la ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba katika mitihani ya taifa.
Mwal. Siame amewadhihirishia wazazi na walezi pamoja na wageni waalikuwa kuwa ufaulu wa wanafunzi katika shule hiyo umekuwa mara zote uwe wa alama “A”, ufaulu huo mara zote umekuwa ndio dira yao kwa kuhakikisha wanapunguza ufaulu wa alama  “B” na ikiwezekana usiwepo ufaulu wa alama “C” na “D”.
Katika matokeo ya mwaka 2016, Mwalimu Mkuu huyo alisema kuwa wanafunzi wa darasa la saba waliofanya mtihani wa kitaifa wamefaulu vizuri ambapo shule hiyo imekuwa ya nne kiwilaya, ya 17 kimkoa na y a 53 kitaifa kati ya shule 8,109.
Akionyesha mtiririko wa ufaulu mwalimu Siame alisema kuwa mwaka 2013 shule hiyo ilikuwa na watahiniwa 32 wanafunzi wane tu ndio walipata alama “A”, mwaka 2014 kulikuwa na watahiniwa 49, wanafunzi 20 walipata alama “A”, mwaka 2015 kulikuwa na watahiniwa 57, wanafunzi 40 walipata alama “A” na mwaka 2016 kulikuwa na watahiniwa 65, wanafunzi 49 walipata alama “A” na wanafunzi 16 walipata alama “B” wakati hakuna mwanafunzi aliyepata alama “C) na “D”.
Mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano mzuri kati ya wanafunzi, wazazi na uongozi wa shule kwa kuwapatia wanafunzi malezi na usimamizi mzuri bora hatua ambayo ndio imekuwa kichocheo cha ufaulu huo.

Comments