TAASISI ZA SERIKALI ZAOMBA VIWANJA DODOMA

By Elias Msuya, MwananchiDodoma. Kaimu Mkurugenzi wa Ardhi na Mkuu wa kitengo cha upimaji wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA), Frank Mkomochi amesema mpaka sasa kuna maombi yanayokaribia kufikia 40 kutoka taasisi za Serikali zinazotaka viwanja vya kujenga ofisi.
“Ni kweli, maombi yameongezeka kutoka kwa taasisi za Serikali na watu binafsi wakitaka kujenga ofisi na uwekezaji. Mpaka sasa maombi yanakaribia 40 kwa taasisi za Serikali, lakini kuna maombi mengi yanaendelea kumiminika kutoka kwa watu binafsi,” amesema Mkomochi.
Mkurugenzi huyo amesema kutokana na hali hiyo, kumekuwa na ongezeko la matapeli wa ardhi wanaonunua viwanja vingi kwa lengo la kuvilangua baadaye.
SOURCE: MWANANCHI