Featured Post

DC MTATURU AMALIZA MGOGORO KATI YA MWEKEZAJI NA WANANCHI

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mang’onyi wakati wa kutatua mgogoro kati ya wananchi na muwekezaji Shanta Gold Mine.
Wanachi Kijijini Mang’onyi wakisikiliza kwa makini maelezo ya Mkuu wao wa Wilaya
Baadhi ya viongozi wakisikiliza maelezo ya awali katika ufunguzi wa mkutano huo uliodumukwa zaidi ya masaa matatu
Dc Mtaturu akikemea tabia ya wanasiasa kutoa matamko ya kisiasa kwa maslahi yao binafsi huku wakiwa mbali na eneo la wawakilishi wao
Wananchi wakimlaki Mkuu wao wa Wilayaya Ikungi
Dc Mtaturu akikemea tabia ya wananchi kuwachagua viongozi ambao wakipewa ridhaa tu wanahamia Dar es salaam ilihali wananchi wao wanabaki kuteseka pasina kuona umuhimu wa viongozi wao
Dc Mtaturu akitoa agizo kwa muwekezaji Shanta Gold Mine kuwalipa fidia haraka wananchi ili mradi huo uanze haraka iwezekanavyo
Nyumbani ni salamu na unyumbani ni kuongea Kinyumbani, moja ya tabasamu kati ya mwananchi na Dc wake wakizungumza kwa lugha moja baada ya mkutano
Wananchi wakielemishwa na Mkuu wa wilaya juu ya siasa zinazokwamisha maendeleo yao huku wanasiasa wenyewe wakishindwa kufanya uwakilishi katika maeneo yao badala yake wamekuwa wawakilishi wa kitaifa
Msingi wa kikao ni kusikilizana Mkuu wa Wilaya ya ikungi Miraji jumanne Mtaturu, Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya, Uongozi wa Shanta Gold Mine na wananchi Kijijini Mang’onyi wakiwa kwenye mkutano wa kutatua mgogoro wao.

Na Mathias Canal, Singida
Mgogoro uliodumu katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi kati ya wananchi wa Kijiji cha Mang'oni na Muwekezaji Shanta Gold Mine umechukua sura mpya ya maelewano baada ya wananchi kupatiwa elimu kuhusu umuhimu wa uwekezekezaji na fursa watakazozipata ikiwa ni pamoja na ajira kwa wananchi wenyewe na maendeleo ya Vijiji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa na Taifa.

Akiwa katika kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amezungumza na wananchi hao kujua kadhia iliyopelekea kutoelewana kwa kipindi chote hicho jambo ambalo limerudisha nyuma maendeleo tarajiwa kwa pande zote mbili.

Mgogoro huo umemalizika kwa Mkuu huyo kuamua kuwa wananchi walipwe fidia haraka iwezekenavyo ili kupisha uanzishwaji wa Mgodi huo ambapo tayari takribani wananchi 67 watalipwa katika awamu ya kwanza huku wengi zaidi 130 kulipwa katika awamu ya pili.

Dc Mtaturu amefanya mkutano wake wa hadhara wa mwanzo tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi ambapo amewaagiza wawekezaji hao kukutana na kuwa na kikao cha pamoja kati yao na wananchi waliofanyiwa tathmini kwa ajili ya makubaliano ya namna bora ya malipo yao ikiwa ni pamoja na kuwashauri kila mmoja kufungua Account Bank ili iwe rahisi na salama katika uhifadhi wa fedha zao.

Baadhi ya Wananchi katika kijiji hicho cha Mang'oni hivi karibuni walizuia njia kwa kuweka magogo na mawe barabarani kama ishara ya kuwazuia wawekezaji hao kupita katika eneo lao kwa madai ya kutolipwa fidia kwa wakati na mwekezaji kuweka alama za mipaka ya eneo lake pasina wananchi kushirikishwa.

Hata hivyo Dc Mtaturu alisema kuwa huenda wananchi walikuwa na hoja ya msingi lakini kutolipwa fidia hakumfanyi mtu kupata uhalali wa kuharibu mali za muwekezaji kwani kufanya hivyo ni sehemu mojawapo inayochelewesha ulipaji wa fidia.

Mtaturu ameonyesha kukerwa na viongozi wanaowapotosha wananchi hao ilihali wakiwa wamejificha ama wanaishi mbali na kijijini hapo na kusema kuwa hiyo ni nidhamu ya woga kwani muwakilishi mzuri wa wananchi ni yule anayetanguliza maslahi ya wananchi mbele kuliko masalahi ya kisiasa, Chama ama maslahi yake binafsi.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa kiongozi mzuri daima ni yule anayetatua changamoto za wananchi sio kuzipinga kwani siasa safi na nzuri ni ile inayoleta maendeleo sio kupinga maendeleo.
Amewataka wawekezaji hao kuwa na mahusiano mazuri na wananchi kwani unapokuwa na mradi wako katika Kijiji chochote nchini usipokuwa na mawasiliano mema na wananchi wa eneo husika ni dhahiri kuwa mradi wako utakuwa hauna tofauti na mradi mfu.

Hata hivyo pamoja na faida kwa wananchi kulipwa fidia na serikali kupata pato lake lakini wananchi 60 kutoka Kijijini hapo wataajiriwa katika Mradi huo kati ya ajira 120 zilizopo ambapo wengine 60 watatoka nje ya eneo hilo ili kutoa fursa kwa watanzania wote kujipatia ajira.

Comments